IMEWEKWA SEPTEMBA 14, 2013 SAA 4:25 USIKU
KOCHA Jose Mourinho amepata kipigo cha kwanza katika ujio wake wa pili Chelsea baada ya bao pekee la Steven Naismith dakika ya 45 na ushei kuipa Everton ushinsdi wa 1-0 katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo.
Kikosi cha Everton kilikuwa: Howard, Coleman, Jagielka, Distin, Baines, Osman, Barry, Mirallas/Deulofeu dk90, Barkley, Jelavic/McCarthy dk66, Naismith/Stones dk89.
Chelsea: Cech, Ivanovic, Luiz, Terry, Cole/Torres dk69, Mikel, Ramires, Schurrle/Lampard dk57, Mata dk5/Oscar dk57, Hazard na Eto'o.
Mshindi: Nyota wa Everton, Steven Naismith akishangilia bao lake pekee lililoizima Chelsea Uwanja wa Goodison Park
Kichwa maridadi: Naismith akiifungia Everton bao pekee
Amepagawa: Samuel Eto'o hakuwa na mwanzo mzuri Chelsea ikifungwa na Everton
Eto'o akipambana
Gareth Barry alifanya vizuri leo akiichezea kwa mara ya kwanza Everton baada ya kujiunga nayo akitokea Manchester City
Majibu yoyote? Jose Mourinho amepata kipigo cha kwanza leo, Chelsea ikilala mbele ya Everton
Andre Schurrle akisikitika baada ya kupoteza nafasi ya kuifungia bao Chelsea kipindi cha kwanza