Na Mahmoud Zubeiry, Mbeya, IMEWEKWA SEPTEMBA 16, 2013 SAA 11:45 JIONI
KOCHA Mkuu wa mabingwa wa soka Tanzania Bara, Yanga SC, Mholanzi Ernie Brandts amesema kwamba anapenda kunywa bia ya Kilimanjaro Premium Lager popote nchini kwa sababu ni bora, ina ladha nzuri na imetulia.
Akizungumza wakati wa ziara ya kikosi chake katika kiwanda cha Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) mjini hapa, beki huyo wa zamani wa kimataifa wa Uholanzi, Brandts alisema kwamba tangu amekuja Tanzania bia yake ni Kilimanjaro tu.
“Ni bia iliyotulia, ina ladha nzuri, ninaipenda na wakati wa mapumziko, huwa ninakunywa hiyo tu,”alisema.
Kikosi cha Yanga leo mchana kilifanya ziara kiwanda cha TBL hapa Mbeya, kilichopo maeneo Iyunga. Katika ziara hiyo, wachezaji walipata fursa ya kujionea mambo mbalimbali, ikiwemo mfumo mzima wa utayarishwaji bia hadi kupakiwa tayari kuingia sokoni.
Walipata fursa ya kuuliza maswali mbalimbali wakati wanatembezwa kwenye kiwanda hicho na wafanyakazi wa TBL Mbeya na kwa ujumla ilikuwa ziara yenye maufaa kwao.
Wafanyakazi wa TBL Mbeya walifurahi kukutana na wachezaji wa Yanga na wengine walichukua fursa hiyo kupiga nao picha za ukumbusho.
Kwa upande wake, Meneja Matukio wa Kampuni hiyo mjini hapa, Godfrey Mwangungula alisema kwamba kiwanda cha TBL Mbeya kinashikilia tuzo ya kiwanda bora Afrika kwa miaka mitatu mfululizo- hivyo ni faraja kwao kutembeleaa na mabingwa wa Tanzania.
Yanga kwa pamoja na wapinzani wao wa jadi, Simba SC na timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars- wote wanadhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premiem Lager inayozalishwa na TBL.
Yanga iko hapa Mbeya tangu Jumatano kwa ajili ya mechi zake mbili za Ligi Kuu dhidi ya timu za hapa. Mchezo wa kwanza ilicheza Jumamosi Uwanja wa Sokoine na kulazimishwa sare ya 1-1 na Mbeya City wakati keshokutwa itahitimisha mechi zake za hapa kwa kumenyana na Prisons kwenye Uwanja huo huo.

Mtaalamu wa ubora upande wa upishi wa bia, Sofia Mvungi (kulia) akimuelekeza jambo kocha wa Yanga SC, Ernie Brandts wakati wa ziara ya timu hiyo kiwanda cha TBL mjini Mbeya leo. |
Kikosi cha Yanga leo mchana kilifanya ziara kiwanda cha TBL hapa Mbeya, kilichopo maeneo Iyunga. Katika ziara hiyo, wachezaji walipata fursa ya kujionea mambo mbalimbali, ikiwemo mfumo mzima wa utayarishwaji bia hadi kupakiwa tayari kuingia sokoni.
Walipata fursa ya kuuliza maswali mbalimbali wakati wanatembezwa kwenye kiwanda hicho na wafanyakazi wa TBL Mbeya na kwa ujumla ilikuwa ziara yenye maufaa kwao.
Haruna Niyonzima akivaa kofia maalum kwa ajili ya kuingia kiwandani. |
Haruna Niyonzima na Simon Msuva wakiangalia kifaa cha kupikia bia namna kinavyoipika |
Mrisho Ngassa akiwangoza wenzake kukatiza katika moja ya maeneo ya kiwanda |
Mtaalamu wa mafunzo wa TBL Mbeya, Andrew Sokolo akitoa maelekezo kwa wachezaji na makocha wa Yanga wakati wa ziara ya timu hiyo leo |
Kocha Ernie Brandts akiangalia mashine ya kutunzi vifaa vya usafi ndani ya kiwanda |
Wafanyakazi wa TBL Mbeya walifurahi kukutana na wachezaji wa Yanga na wengine walichukua fursa hiyo kupiga nao picha za ukumbusho.
Kwa upande wake, Meneja Matukio wa Kampuni hiyo mjini hapa, Godfrey Mwangungula alisema kwamba kiwanda cha TBL Mbeya kinashikilia tuzo ya kiwanda bora Afrika kwa miaka mitatu mfululizo- hivyo ni faraja kwao kutembeleaa na mabingwa wa Tanzania.
Yanga kwa pamoja na wapinzani wao wa jadi, Simba SC na timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars- wote wanadhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premiem Lager inayozalishwa na TBL.
Mtaalamu wa ubora upande wa upishi wa bia, Sofia Mvungi akiwaelekeza mambo wachezaji wa Yanga. Wengine kushoto ni Agnes Mahenge na Beata Mrema. |
Mtaalamu wa Uonjaji wa TBL Mbeya, Maria Samlongo akiwaelekeza mambo wachezaji wa Yanga leo |
Jerry Tegete na Mrisho Ngassa wakielekezwa jambo na Stellah Alexander |
Kipa wa Yanga SC, Deo Munishi 'Dida' akicheza Pool Table katika baa ya Rungwe Pub, iliyopo ndani ya kiwanda cha TBL Mbeya |
Kipa wa Yanga SC, Ally Mustafa 'Barthez' akiteremka kwenye basi baada ya kufika kiwanda cha TBL |
Yanga iko hapa Mbeya tangu Jumatano kwa ajili ya mechi zake mbili za Ligi Kuu dhidi ya timu za hapa. Mchezo wa kwanza ilicheza Jumamosi Uwanja wa Sokoine na kulazimishwa sare ya 1-1 na Mbeya City wakati keshokutwa itahitimisha mechi zake za hapa kwa kumenyana na Prisons kwenye Uwanja huo huo.
Basi la Yanga SC linaingia kiwanda cha TBL Mbeya |
Wa Manungu; Wachezaji wa Yanga SC waliotokea Mtibwa Sugar, kutoka kulia Juma Abdul, Said bahanuzi, Hussein Javu, Deo Munishi 'Dida' na Rajab Zahir. Hapoa amepungua Nizar Khalfan pekee wakiwa TBL leo |
Mtaalamu wa upishi wa pombe, Meshack Mwaluko akimuelekeza jambo David Luhende |
Beki wa Yanga SC, Kevin Yondan akisaini jezi maalum ya Yanga kwa ajili ya wafanyakazi wa TBL Mbeya |