IMEWEKWA SEPTEMBA 24, 2013 SAA 7:02 USIKU
MSHAMBULIAJI Mario Balotelli amefungiwa mechi tatu kufuata kumvaa refa katika mchezo ambao timu yake, AC Milan ilichapwa mabao 2-1 na Napoli Jumapili.
Balotelli, ambaye alikosa na kufunga bao zuri la kufutia machozi kwa timu yake, alionyeshwa kadi ya pili ya njano baada ya mechi kwa kumvaa refa.
Mshambuliaji huyo wa Italia sasa atakosa mechi tatu zijazo kwa kosa hilo.
VIDEO: Scroll down to watch Balotelli miss the first penalty of his career against Napoli
Tulia bwana: Mario Balotelli, kushoto, akitulizwa na mchezaji mwenzake wa Milan, Marco Amelia baada ya kulimwa kadi nyekundu
Kachaa Mario: Baloteli akibishana na refa Luca Banti
Balotelli, ambaye alifunga penalti zake zote 21 za awali katika mechi rasmi, mkwaju wa Jumapili uliokolewa na kipa wa Napoli, Pepe Reina.
Kadi hiyo nyekundu ya utata, inamaanisha Super Mario atakosa mechi na Bologna, Sampdoria na Juventus, ingawa Milan inaweza kukatia rufaa adhabu hiyo.
Anakosa: Mario Balotelli akikosa penalti juzi
Bonge la bao: Lakini Balotelli akafunga kwa tik tak