IMEWEKWA SEPTEMBA 19, 2013 SAA 6:53 USIKU
ARSENAL imeanza vyema Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kushinda ugenini mabao 2-1 dhidi ya wenyeji, Marseille Uwanja wa Velodrome, Ufaransa.
Mabao ya Gunners yalifungwa na Theo Walcott dakika ya 65 na Aaron Ramsey dakika ya 83, wakati la wenyeji lilifungwa na Jordan Ayew kwa penalti dakika ya 90.
Kikosi cha Arsenal kilikuwa: Szczesny, Gibbs, Koscienly, Mertesacker, Sagna, Flamini/Myaichi dk90, Wilshere, Ramsey, Ozil, Walcott/Monreal dk77 na Giroud.
Marseille: Mandanda, Fanni, N'Koulou, Mendes, Morel, Romao, Imbula/Thauvin dk79, Payet/J.Ayew dk72, Valbuena/Khalifa dk89, A. Ayew na Gignac.
Kitu hicho: Theo Walcott ameifungia Arsenal
Kitu kingine: Aaron Ramsey amefunga bao la sita msimu huu
Si mchezo wangu: Mesut Ozil alicheza kiungwana katika ukabaji wake
Kipaji: Theo Walcott akipambana na kiungo wa Marseille, Mathieu Valbuena
Yuko juu: Jack Wilshere alicheza vizuri katika nafasi ya kiungo
Sito rafu? Buti la juu likimuelekea Mathieu Flamini
Rekodi ya klabu: Arsenal imetweet mechi zake 10 ilizoshinda ugenini
Hafunguki kwa urahisi: Steve Mandanda aliibania Arsenal hadi dakika ya 65
Yalaaa: Arsenal walifikiri walistahili kupewa penalti baada ya buti hili alilopigwa Per Mertesacker
Yuko juu: The Gunners ina sababu za kujivunia Ozil
La kufuta machozi: Jordan Ayew akifunga kwa penalti
Mchapakazi: Flamini alionyesha yeye ni mchezaji hodari
Mgumu: Arsene Wenger (kulia) atafurahia Mertesacker na Wojciech Szczesny (kushoto) wasiporuhusu mabao
Nambari moja: Walcott akiupungua umati wa mashabiki baada ya mechi
Alipigana: Olivier Giroud alishindwa, kufunga licha ya kupambana