Na Rachel Pallangyo, IMEWEKWA AGOSTI 27, 2013 SAA 9:20 ALASIRI
UONGOZI wa Shirika la Ndege la Oman Air leo umekabidhi seti mbili za jezi kwa timu ya soka ya Gymkhana, kwa ajili ya matumizi katika mechi zao mbalimbali za mashindano na kirafiki.
Meneja wa Oman Air Tanzania, Adil Alzadjali (kulia) akimkabidhi jezi Nahodha wa Gymkhana, Mohamed Seif leo, Dar es Salaam.
Akizungumza leo mjini Dar es Salaam, Meneja Mwakilishi wa shirika hilo hapa nchini, Adil Alzadjali alisema wamekuwa na mahusiano ya muda mrefu na klabu hiyo na lengo la kutoa vifaa hivyo ni kusaidia maendeleo ya mpira hapa nchini, hususani klabu hiyo.
“Bado tutaendelea kushirikiana kwa karibu na uongozi wa klabu hii, lengo ni kuhakikisha wanafikia malengo yao na kufanya vema katika michezo yao,” alisema Alzadjali.

Kwa upande wa Nahodha wa timu hiyo, Mohamed Seif alitoa shukrani kwa uongozi wa Oman Air kwa jezi walizotoa, kwani zitawasaidia kutimiza malengo yao na pia akasifia mchango wao katika kushirikiana na uongozi mzima wa klabu ya Gymkhana.
UONGOZI wa Shirika la Ndege la Oman Air leo umekabidhi seti mbili za jezi kwa timu ya soka ya Gymkhana, kwa ajili ya matumizi katika mechi zao mbalimbali za mashindano na kirafiki.
![]() |