IMEWEKWA AGOSTI 21, 2013 SAA 4:00 ASUBUHI
KLABU ya Manchester United ilianza Ligi Kuu Egland kwa ushindi mnono wa mabao 4-1 dhidi ya Swansea Jumamosi na ikaonekana kikosi kipo kamili.
Lakini vijana wa David Moyes walionekana Jijini jana usiku kwa mtoko wa chakula cha pamoja kama timu, wakitoka na wake zao na mahawara.
Huku tetesi zikiuzunguka mustakabali wake katika klabu hiyo, mshambuliaji Wayne Rooney alitoka na mkewe Coleen, na kupunguza shaka juu ya mustakabali wake katika klabu.
Mtoko na mama watoto: Rooney akiwasili na mkewe Coleen (kushoto), wakati Moyes akionekana poa baada ya ushindi wa pili kazini
Katikati ya mji: Johnny Evans akiwasili na mkewe Helen McConnell (kushoto), wakati Nemanja Vidic akitembea na mkewe, Ana Ivanovic huko Deansgate, Manchester
Rooney aliungana na Moyes pamoja na wachezaji wenzake wakiwemo Rio Ferdinand, Nemanja Vidic, Danny Welbeck, Wilfried Zaha na Tom Cleverley huko Deansgate katikati ya mji wa Manchester.
Wakati nyota wa Ligi Kuu wakitembea kwenda kukutana na wachezaji wenzao wa United, beki wa kati, Ferdinand alizuiwa na wapita njia kwa ajili ya kupiga nao picha.
Kocha wa Chelsea, Mourinho tayari amekwishatuma ofa mbili kwa ajili ya Rooney, lakini amesistiza kupigania saini ya mchezaji huyo wa England hadi mwisho.
Mapema jana, alisema: 'Wakati unafikiri ungependa kuwa na mchezaji mmoja na soko liko wazi na ofa rasmi haijatolewa, ofa rasmi wakati wote inakubaliwa katika njia za kimaadili, unajaribu kwa sababu hakuna anayekuzuia kujaribu.
Nafasi ya picha;Rio Ferdinand akipiga picha na shabiki huko Deansgate, Manchester
Beki Chris Smalling (kushoto) akiwasili na mpenzi wake, na kiungo Tom Cleverley (kulia) na hawara yake, Georgina Dorsett
Kila mtu na wake: Robin na Bouchra van Persie (kushoto) akiwasili na kulia ni Ryan na Stacey Giggs
Masela: Danny Welbeck, Wilfried Zaha, David De Gea na Antonio Valencia wakitembea
Miamba: Alexander Buttner, Rio Ferdiand na Shinji Kagawa wakiwasili kwa chakula cha timu mjini Manchester
Kwa raha zao: Ashley Young (kushoto) na Phil Jones (kulia) 
Ushindi wa kwanza: United wakishangilia baada ya kuifunga Swansea 4-1 Jumamosi