// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); MAZOEZI YA MWISHO AZAM FC KABLA YA KUIVAA RHINO KESHO, BOCCO NJE, KARIHE NA NYONI 'TIA TIA MAJI' - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE MAZOEZI YA MWISHO AZAM FC KABLA YA KUIVAA RHINO KESHO, BOCCO NJE, KARIHE NA NYONI 'TIA TIA MAJI' - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

        Tuesday, August 27, 2013

        MAZOEZI YA MWISHO AZAM FC KABLA YA KUIVAA RHINO KESHO, BOCCO NJE, KARIHE NA NYONI 'TIA TIA MAJI'

        IMEWEKWA AGOSTI 27, 2013 SAA 11:48 JIONI
        Kocha Mkuu wa Azam FC, Muingereza Stewart John Hall akimpa maelekezo mchezaji wake, kiungo Khamis Mcha 'Vialli' kwenye Uwanja wa Ally Hassan Mwinyi mjini Tabora jioni ya leo. Azam itamenyana na wenyeji Rhino Rangers kesho kwenye Uwanja huo katika mfululizo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara. 

        Mshambuliaji Seif Abdallah Karihe akitibiwa na daktari wa timu, Vincent Madege baada ya kuumia kifundo cha mguu mazoezini leo

        Beki Erasto Nyoni akipewa mazoezi mepesi na Dk, Madege leo

        Kikao cha dharula; Kocha Stewart Hall akijadiliana na wasaidizi wake Ibrahim Shikanda kulia na Kali Ongala kushoto wakati wa mazoezi leo

        Beki Agrey Morris kulia akimtoka mshambuliaji Kipre Tchetche mazoezini leo

        Beki David Mwantika akimtoka Khamis Mcha Vialli nyuma yake. Wengine nyuma ni Waziri Salum na kulia ni Jabir Aziz

        Injini ya timu; Salum Abubakar 'Sure Boy' yuko fiti kabisa kwa mchezo wa kesho

        Mlinzi Mkuu; Beki wa kati Aggrey Morris yuko tayari kwa shughuli ya maafande wa JWTZ kesho

        Jabir Aziz kushoto akiwania mpira na Mudathir Yahya

        Kocha Msaidizi, Kali Ongala alishiriki mazoezi 

        John Bocco 'Adebayor' alikuwa nje kabisa akipiga stori na Meneja Jemadari Said kwa sababu ya maumivu

        Himid Mao akijimwagia maji mazoezini leo

        • Blogger Comments
        • Facebook Comments
        Item Reviewed: MAZOEZI YA MWISHO AZAM FC KABLA YA KUIVAA RHINO KESHO, BOCCO NJE, KARIHE NA NYONI 'TIA TIA MAJI' Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry