IMEWEKWA AGOSTI 20, 2013 SAA 6:50 MCHANA
KLABU ya Manchester United inajiandaa kupeleka ofa ya pili ya Pauni Milioni 35 kwa ajili ya wachezaji wawili wa Everton, Leighton Baines na Marouane Fellaini.
Mabingwa hao wa Ligi Kuu ya England ofa yao ya awali ya Pauni Milioni 28 ilipigwa chini na Everton jana.
Klabu hiyo ya Merseyside inaonekana haitaki kuwauza wachezaji hao, lakini kocha wa United, David Moyes – ambaye aliondoka Goodison Park kuhamia Old Trafford majira haya ya joto- amedhamiria kusajili wachezaji wapya na anataka klabu yake itilie mkazo.
Ofa: Kocha wa Manchester United, David Moyes ataongeza dau kwa ajili ya Marouane Fellaini na Leighton Baines
Pigwa chini: Everton ilikataa ofa ya awali ya United kwa ajili ya Baines na Fellaini, pichani akiichezea klabu hiyo Jumamosi
Mlengwa: Moyes anataka kumchukua Fellaini akafanye naye kazi Old Trafford, lakini atatakiwa kuongeza dau kuinasa saini ya Mbelgiji huyo
Huku Everton ikipiga thamani ya Pauni Milioni 40 kwa wachezaji wote hao, United inapambana kuhakikisha inawapata wachezaji hao kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili.
Pamoja na hayo, inafahamika watapeleka ofa ya Pauni Milioni 35. Hiyo itatokana na kumthaminisha Baines kwa Pauni Milioni 12 na Fellaini Pauni Milioni 23.
Wawili muhimu: Baines na Fellaini ndio wachezaji bora Everton na klabu hiyo inawathaminisha kwa Pauni Milioni 40