IMEWEKWA AGOSTI 25, 2013 SAA 3:08 USIKU
MABAO mawili ya kichwa dakika za lala salama ya Fraizer Campbell tyameipa Cardiff ushindi wa kwanza katika Ligi Kuu ya England, baada ya kuilaza Manchester City 3-2.
Edin Dzeko alitangulia kuifungia timu ya Manuel Pellegrini dakika ya 52, lakini Cardiff ikasawazisha kupitia kwa Aron Gunnarsson dakika ya 60, kabla ya Campbell kufunga dakika za 79 na 87.
Alvaro Negredo akafungua akaunti yake ya mabao City kwa bao la dakika ya mwisho kabisa.
Kikosi cha Cardiff City kilikuwa: Marshall; Connolly, Caulker, Turner, Taylor, Bellamy/Cowie dk83, Gunnarsson, Kim/Mutch dk90, Medel, Whittingham na Campbell/Cornelius dk90.
Manchester City: Hart, Zabaleta, Garcia, Lescott, Clichy, Navas/Nasri dk55, Fernandinho/Milner dk77, Toure, Silva, Aguero na Dzeko/Negredo dk69.
Dogo noma: Frazier Campbell amefunga mabao mawili Cardiff ikiibwaga Manchester City
Shuti hadi bao: Edin Dzeko akifunga
Kifaa: Fraizer Campbell akimruka kipa wa City, Joe Hart
Hapa ni namna Alvaro Negredo alivyoifungia Manchester City bao la pili - Gonga hapa kupata zaidi yaliyojiri Uwanja wa Cardiff City
Mpambano kwenye kiungo: Kiuno wa Cardiff, Gary Medel akipambana na kiungo wa City, Fernandinho
Kizaazaa: Mabeki wa City wakiwa wameduwaa baada ya Aron Gunnarsson kusawazisha
Amepagawa: Sergio Aguero haamini kipigo
Shujaa: Fraizer Campbell ameing'arisha timu mpya katika Ligi Kuu
Hatari: Alvaro Negredo alifunga dakika ya mwisho
Wakati wa kusherehekea: Mashabiki wa Cardiff wakishangilia bao la Campbell
Majanga: Alvaro Negredo akisikitika chini
Kipa bomu: Joe Hart ameonyesha tena hayuko katika kiwango kizuri
Shujaa wa United? Campbell ametokea kwenye akademi ya Old Trafford