// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); LIVERPOOL KUZIPIGA BAO MAN UNITED NA SPURS KATIKA KINYANG'ANYIRO CHA SAINI YA WILLIAN - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE LIVERPOOL KUZIPIGA BAO MAN UNITED NA SPURS KATIKA KINYANG'ANYIRO CHA SAINI YA WILLIAN - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

        Saturday, August 17, 2013

        LIVERPOOL KUZIPIGA BAO MAN UNITED NA SPURS KATIKA KINYANG'ANYIRO CHA SAINI YA WILLIAN

        IMEWEKWA AGOSTI 17, 2013 SAA 2:35 ASUBUHI
        KLABU ya Liverpool imekaa katika mkao wa kula saini ya Willian na kuzipiku Tottenham na Manchester United ambazo pia zinawania saini ya mchezaji huyo mwenye thamani ya Pauni Milioni 30.
        Zote Liverpool na Tottenham zimeingia kwenye mazungumzo na Anzhi Makhachkala kwa ajili ya mwanasoka huyo wa kimataifa wa Brazil, lakini inatokea Willian amekaa kwenye mkao wa kuelekea zaidi Anfield.
        Ikiwa Liverpool itakamilisha uhamisho wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25, Willian atakuwa mchezaji wa pili katika klabu hiyo kihistoria na atakuwa mchezaji babu mkubwa ambaye amesajiliwa na kocha Brendan Rodgers majira haya ya joto.
        On the move: Willian seems set to leave Anzhi and Liverpool are closing in on his signature
        Njiani: Willian anajiandaa kuondoka Anzhi na Liverpool ipo karibu kumnasa
        Na itakuwa na maana kubwa kwa Liverpool, kuwapiga bao wapinzani wao wakubwa Manchester United pamoja na Tottenham, ambao wanamtamanisha kucheza michuano ya Ulaya ili avutike zaidi kusaini kwao.
        Willian ameaiambia ESPN Brazil, baada ya kuambiwa Liverpool inamtaka mapema wiki hii kwamba; 'ametulia sana na anasubiri kilicho bora' na pia akaitaka Liverpool kama klabu kubwa.
        Wanted: Brendan Rodgers would love the £30m man to Liverpool's squad
        Anamtaka: Brendan Rodgers anaweza kutoa Pauni Milioni 30 kumuingiza mchezaji huyo kikosini Liverpool
        Rodgers amekuwa akipambana kuboresha kikosi chake kutafuta viwango vya kuiwezesha timu kufuzu michuano ya na kuwasili kwa Willian, ambaye alishinda Kombe la UEFA enzi zake akiichezea Shakhtar Donetsk, kunaweza kusababisha hali hiyo. 
        Liverpool pia itamsajili beki wa kushoto anayecheza kwa mkopo wa muda mrefu Valencia, Aly Cissokho akifuzu vipimo vya afya.
        Missing out: David Moyes has been foiled in the transfer marker this summer
        Wanamkosa: David Moyes amekula za uso sana katika dirisha la usajili majira haya ya joto
        • Blogger Comments
        • Facebook Comments
        Item Reviewed: LIVERPOOL KUZIPIGA BAO MAN UNITED NA SPURS KATIKA KINYANG'ANYIRO CHA SAINI YA WILLIAN Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry