IMEWEKWA AGOSTI 30, 2013 SAA 4:37 ASUBUHI
MSIMU uliopita walipokutana kwenye Uwanja wa Emirates na wana fainali ya Ligi ya Mabingwa, Oktoba 22, matokeo yalikuwa Arsenal 0 Borussia Dortmund 0.
Lakini nje ya Uwanja, matokeo mengine yanaleta habari nyingine tofauti.
Kuingia fainali msimu uliopita Uwanja wa Wembley kumempa Jurgen Klopp fungu la kutosha la fedha lililowawezesha kutoa Pauni Milioni 43 kwa ajili ya Pierre-Emerick Aubameyang, Henrikh Mkhitaryan na Sokratis.
Mtihani mgumu: Kocha Arsene Wenger, Arsenal amepangwa na Marseille, Dortmund na Napoli
Mlengwa: Arsenal itatakiwa kula sahani moja na Gonzalo Higuain wa Napoli (kushoto) na Robert Lewandowski wa Dortmund
Wanakutana tena: Kocha Napoli, Benitez atakutana na Wenger kwa mara nyingine
Yuko safi: Jurgen Klopp wa Dortmund, aliyemaliza nafasi ya pili msimu uliopita, amepangwa na Arsenal
Watamenyana na wachezaji wapya wa Arsenal, waliosajiliwa majira haya ya joto — Mathieu Flamini na Yaya Sanogo, wachezaji wawili ambao hawakugharimu sana katika uhamisho wao.
Hali hii inaonyesha ni kiasi gani Arsenal, wapo katika kundi gumu H dhidi ya Dortmund, Rafa Benitez na Napoli na Marseille.
Dhidi ya Napoli watakabiliana na Gonzalo Higuain, aliyesajiliwa kwa Pauni Milioni 34 kutoka Real Madrid, mshambuliaji ambaye Arsenal pia walimfukuzia sana wakaishia kunawa.
Dortmund imekuwa na mwanzo mzuri ikilipa kisasi cha kufungwa katika fainali ya Ligi ya Mabingwa Mei mwaka huu kwa Bayern Munich, kwa kumfunga Pep Guardiola kocha mpya wa timu hiyo mabao 4-2 katika Super Cup ya Ujerumani.
Wameimarisha timu kwa kuziba pengo la Mario Gotze katika safu ya kiungo kwa kutumia Pauni Milioni 24 kumsaini Mkhitaryan kutoka Shakhtar Donetsk.
Mbele, Robert Lewandowski, ambaye amesaini mkataba wa kuendelea kufanya kazi kwa msimu mmoja zaidi, tayari amefunga mabao matatu msimu huu.
Majina makubwa: Neymar (kushoto) na Lionel Messi wote watasafiri kwenda Glasgow na Barcelona
Usiku wa kukumbukwa: Celtic iliifunga Barcelona 2-1 mwaka jana
Anarudi Uingereza: Mshambuliaji wa AC Milan, Mario Balotelli atakutana na Celtic
Wenger ana kibarua cha kupigana kukusanya pointi 10 mapema, ili kujihakikishia anaingia kwenye droo ya hatua ya mtoano Desemba.
Awali, itashuhudiwa Manchester City wakirejea Uwanja wa Allianz-Arena kumenyana na Bayern. Mengi yamebadilika tangu usiku wa Septemba 2011 wakati Carlos Tevez alipogombana na kocha wa zamani wa City, Roberto Mancini kwenye mstari wa kuinia uwanjani.
MAMBO MUHIMU KUJUA KUHUSU LIGI YA MABINGWA
ARSENAL
- Arsenal haijawahi kupoteza mechi ya ugenini Ufaransa (imeshinda 6, sare 4, ukiondoa mechi za kukutana wageni wenzao huko).
- Arsenal imeshinda mechi zote za nyumbani awali dhidi ya Borussia Dortmund katika Ligi ya Mabingwa, ikifunga mabao manne.
- The Gunners imecheza mechi sita bila kufungwa katika mechi nane zilizopita za Ligi ya Mabingwa.
CELTIC
- Celtic imeshinda mechi mbili kati ya nne zilizopita za nyumbani Ligi ya Mabingwa dhidi ya Barcelona, ikiwemo ya ushindi wa 2-1 Uwanja wa Parkhead msimu uliopita.
- The Bhoys hawajashinda hata mechi moja katika 10 zilizopita za ugenini dhidi ya timu za Italia, ikitoa sare tatu na kufungwa saba. Ugenini dhidi ya AC Milan, Celtic imetoa sare moja na kufungwa tatu. Celtic haijafungwa katika mechi tatu zilizopita Ulaya, ilipokutana na timu za Uholanzi, ikishinda mbili na kutoa sare moja.
CHELSEA
- Chelsea imeshinda mechi sita na kufungwa moja katika ya saba za Ligi ya Mabingwa nyumbani dhidi ya timu za Ujerumani, ikicheza mechi sita bila kuruhusu nyavu zake kuguswa na kufungwa mabao mawili katika mechi zote hizo.
- Kabla ya ushindi wao na FC Basel msimu uliopita, Chelsea ilitolewa na timu ya Usiwsi kwa kufungwa 2-1 jumla na FC St Gallen msimu wa 2000/2001 katika Raundi ya kwanza ya Kombe la UEFA.
- Chelsea imeshinda mechi zake zote za awali nyumbani dhidi ya timu za Romania, lakini haijawahi kushinda Romania katika mechi za Ulaya (ikitoa sare moja na kufungwa moja).
MANCHESTER CITY
- City ilicheza na Bayern katika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa 2011-2012, ikifungwa 2-0 ugenini na kushinda 2-0 nyumbani. Inakumbukwa sana Carlos Tevez aligoma kupasha misuli moto kuingia dakika za mwishoni kwenye mechi ya ugenini.
- Man City haijawahi kucheza na timu ya Urusi wala Czech kwenye mashindano ya Ulaya. Msimu uliopita, Man City iliweka rekodi ya kuwa timu ya kwanza England katika historia ya Ligi ya Mabingwa kushindwa kushinda japo mchezo mmoja wa hatua ya makundi.
MANCHESTER UNITED
- Manchester United imeshinda mechi tatu na haijafungwa katika mechi zake za awali dhidi ya timu za Ukraine kwenye mashindano ya Ulaya.
- Man Utd imeshinda mechi moja katia ya nane zilizopita za Ulaya nchini Hispania (sare nne na kufungwa tatu).
- United imefungwa mechi mbili katika mechi zake 14 dhidi ya timu za Ujerumani na kushinda nane na sare nne.
Usikuwa wa ufalme: Mabingwa wa Ulaya, Bayern Munich watamenyana na Manchester City
Mtu mpya: Kocha mpya wa Bayern, Pep Guardiola atakuwa kazini Uwanja wa Etihad atakapomenyana na Manchester City
Mlengwa: Manuel Pellegrini atapenda kuiongoza Manchester City kusonga mbele hatua ya 16 Bora Ligi ya Mabingwa kwa mara ya kwanza
NCHI ZILIZOTOA MABINGWA ULAYA NA IDADI ZAKE:
Hispania: Mara 13; Real Madrid 9, Barcelona 4
Italia: Mara 12; Milan 7, Inter 3, Juventus 2
England: 12 Liverpool 5, Man Utd 3, Nottm Forest 2, Chelsea 1, Aston Villa 1
Ujerumani: Mara 7; Bayern 5, Dortmund 1, Hamburg 1
Uholanzi: Mara 6; Ajax 4, PSV 1, Feyenoord
Ureno: Mara 4; Porto 2, Benfica 2
Ufaransa: Mara 1; Marseille
Scotland: Mara 1; Celtic
Romania: Mara 1; Steaua
Serbia: Mara 1; Red Star Belgrade