IMEWEKWA JULAI 2, 2013 SAA 12:05 ALFAJIRI
KLABU ya Arsenal imethibitisha katika tovuti yake kwamba mwanasoka kinda wa kimataifa wa Ufaransa, Yaya Sanogo amesaini Mkataba wa muda mrefu kwao.
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 20 amejiunga kwa ada ndogo tu baada ya kumaliza Mkataba wake klabu ya Daraja la Kwanza Ufaransa, Auxerre.
Sanogo kwa sasa yupo na timu ya taifa ya vijana ya Ufaransa chini ya umri wa miaka 20, katika Kombe la Dunia la U-20, akiwa amefunga mabao mawili kati ya matatu ya timu yake nchini Uturuki, na amefunga mabao tisa katika mechi 13 katika msimu alioandamwa na majeruhi Ufaransa.
Mlengwa: Sanogo amefanya vitu adimu Ufaransa
Wengi waja? Higuain (kushoto) na Rooney (kulia) nao pia wanafikiriwa kuwa katika orodha ya wachezaji anaowataka Wenger
Gonzalo Higuain na Wayne Rooney ni washambuliaji wengine walioripotiwa kutakiwa The Gunners msimu huu, lakini Wenger anavutiwa mno na uwezo wa Sanogo.
"Sanogo ni usajili mzuri wa kinda kwetu,"aliiambia Arsenal.com. "Ameonyesha uwezo wake siku za karibuni akiwa na Auxerre na poa kikosi cha vijana chini ya miaka 20 cha Ufaransa.
"Tunasonga mbele kwa Yaya kujiunga nasi na kuendeleza kukuza kiwango chake,"alisema Wenger.
Zoezi hilo lipo kwenye kukamilisha taratibu za kawaida za usajili na Sanogo atajiunga na wenzake baada ya mashindano ya Uturuki.