IMEWEKWA JULAI 19, 2013 SAA 2:44 ASUBUHI
KOCHA Arsene Wenger amepewa ruhusa kuamua kuhusu usajili ya Pauni Milioni 40 wa Luis Suarez.
Mshambuliaji huyo wa Liverpool ni kipaumbe cha kwanza katika usajili wa Arsenal majira haya ya joto na timu hiyo ya London tayari imetoa ofa ya awali ya Pauni Milioni 30 iliyokataliwa.
BIN ZUBEIRY imeripoti mapema wiki hii namna ambavyo Gunners wameanza tena mazungumzo na mabosi wa Merseyside juu ya ofa mpya ya Pauni Milioni 35.
Lakini klabu hiyo ya Anfield imeweka wazi kwamba, mchezaji huyo hawezi kupatikana chini ya bei wanayoitaka.
Mkwanja mrefu: Arsene Wenger amepewa ruhusa kutumia Pauni Milioni 40 kwa ajili ya Luis Suarez
Ofa ya Pauni Milioni 40 litakuwa jaribio tosha la kumng'oa Suarez anayetaka kuondoka Anfield majira haya ya joto.
Wakala wa Suarez, Pere Guardiola, alikuwa na majadiliano na Liverpool ambayo imekubali kusikiliza ofa.
Ofa hiyo itakuwa uamuzi mzito kwa Gunners ambao wanataka kumnasa mchezaji huyo mmoja kati ya watatu inayowataka sana.
Sambamba na Suarez, Wenger pia anafikiria kuwasajili Gonzalo Higuain na Wayne Rooney.
Sokoni: Wakala wa Suarez amesema ikiwa Arsenal itatoa ofa, Liverpool watatakiwa kuwasikiliza
Amerudi kazini: Brendan Rodgers na Liverpool wamerejea kwenye mazoezi ya kujiandaa na msimu
Kocha wa Liverpool, Brendan Rodgers anaamini Suarez ana deni ka wachezaji wenzake - na mashabiki wa klabu - la kubaki Anfield.
"Si kuhusu mimi au klabu, nafikiri mashabiki na wachezaji wenzake kwa kile wanachompa,"alisema.
"Wamekuwa naye kwa shida na raha, na kwa vipindi vyote alivyopitia kwa misimu zaidi iliyopita. Ikiwa kuna yeyote anayedai, ni wao ni wachezaji wenzake, ambao walipambana upande wake, hakika si mimi,".
Anateka hisia: Suarez amesema anapagawa na mpango wa kusajiliwa na wapinzani wa Liverpool katika Ligi Kuu England, Arsenal
Arsene Wenger akiwa kwenye ziara ya timu kujiandaa na msimu
Shakani: Usajili wa Higuain unaweza kukwama, na Wenger amehamishia mawindo yake sehemu nyingine
Wakati huo huo, beki wa Gunners, Bacary Sagna amesema hataondoka Arsenal - na anataka kuthibitisha anastahili Mkataba mpya.
Sagna, mwenye umri wa miaka 30, yupo katika miezi 12 ya mwisho ya Mkataba wake na ana ofa kutoka Paris Saint Germain, Anzhi na klabu za Mashariki ya Kati.
Mfaransa huyo amegoma kusaini Mkataba wa mwaka mmoja zaidi, akiamini anastahili Mkataba mrefu na anajiandaa kuondoka kama mchezaji huyu mwishoni mwa msimu.
Lakini licha ya utata wa Mkataba wake, Sagna amesema anataka kubaki Uwanja wa Emirates na kuthibitisha anastahili Mkataba wa maana.
"NafuraI kuchezea Arsenal. Naipenda timu yangu, najitolea kwa asilimia 100 kwa ajili ya timu na wakati wote naifanyoa mazuri. Bado nipo hapa.
Hapa pa kubaki: Bacary Sagna amesema anataka kubaki Arsenal