Na Mahmoud Zubeiry, IMEWEKWA JULAI 13, 2013 SAA 11:40 JIONI
BAO pekee la Dennis Iguma dakika ya 46 jioni hii limeiwezesha Uganda kuibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Tanzania kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kujiweka katika nafasi nzuri ya kusonga mbele kwenye michuano ya Ubingwa wa Mataifa wa Mataifa Afrika (CHAN), inayohusisha wachezaji wanaocheza ligi za nchini mwao pekee.
Iguma aliifungia The Cranes bao hilo, baada ya kutokea piga nikupige langoni mwa Stars kufuatia krosi maridadi ya Brian Majwega, ambaye leo alikuwa mwiba mkali kwa Taifa Stars.
Hadi mapumziko hakuna timu iliyofanikiwa kuona lango la mwenzake na kwa ujumla katika dakika zote hizo 45 hakukuwa na shambulizi la kutisha kwa pande zote.
Brian Majwega alifanikiwa kumgeuza uchochoro Erasto Nyoni na kuingia ndani mara kadhaa, lakini pasi na krosi zake ziliokolewa na mabeki wa Stars inayofundishwa na Mdenmark, Kim Poulsen.
Mrisho Ngassa alipewa mipira mirefu kadhaa, lakini mabeki wa Uganda wakiongozwa na mkongwe, Nahodha wao, Hassan Wasswa walisimama imara kumdhibiti.
Mashambulizi mengine ya Stars yalipitia kwa John Bocco ‘Adebayor’, ambaye alikuwa anapigiwa mipira mirefu, lakini alidhibitiwa pia. Timu zote zilicheza sawa kipindi cha kwanza.
Kipindi cha pili timu zote zilifanya mabadiliko, Stars ikiwapumzisha beki Erasto Nyoni na kiungo Mwinyi Kazimoto na kuwaingiza David Luhende na Haroun Chanongo, lakini walikuwa ni Uganda wanaofundishwa na makocha wa zamani wa klabu ya Yanga, Mserbia Milutin Sredojevic ‘Micho’ anayesaidiwa na Sam Timbe waliobuka vinara.
Lakini baada ya kufungwa Stars, waliongeza kasi na nguvu ya uchezaji na kufanikiwa tu kulitia misukosuko lango la Uganda na si kupata bao japo la kusawazisha.
Matokeo hayo yanamaanisha Stars itahitaji kushinda ugenini kuanzia mabao 2-0 wiki mbili zijazo ili isonge mbele, vinginevyo itakuwa imetupwa nje ya mashindano hayo.
Katika mchezo wa leo kikosi cha Stars kilikuwa; Taifa Stars; Juma Kaseja, Erasto Nyoni/David Luhende, Shomary Kapombe, Aggrey Morris, Kevin Yondan, Frank Domayo, Amri Kiemba, Salum Abubakar, John Bocco ‘Adebayor’, Mwinyi Kazimoto/Haruna Chanongo na Mrisho Ngassa.
The Cranes; Hamza Muwonge, Hassan Wasswa, Nico Wadada, Brian Majwega, Savio Kabugo, Richard Kasaga, Dennis Iguma, Said Kyeyune, Joseph Mpanda, Patrick Edema/Ivan Ntege na Tonny Odur/Frank Kalanda.

![]() |
Anapasua msitu; Kiungo wa Tanzania, Amri Kiemba akipasua ngome ya Uganda katika mchezo wa leo Uwanjqa wa Taifa, Dar es Salaam. |

Kiembaa huyoo... |
![]() |
Kiemba hatari, lakini mabao yalikataa leo |