// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); SIMBA SC KUSHIRIKI MASHINDANO YA KILIMO KENYA, KIGGI KUTIBIWA INDIA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE SIMBA SC KUSHIRIKI MASHINDANO YA KILIMO KENYA, KIGGI KUTIBIWA INDIA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Thursday, July 04, 2013

    SIMBA SC KUSHIRIKI MASHINDANO YA KILIMO KENYA, KIGGI KUTIBIWA INDIA

    Kiggi Makassy
    Na Mahmoud Zubeiry, IMEWEKWA JULAI 4, 2013 SAA 8:15 MCHANA
    WAKATI Simba SC imealikwa kushiriki michunao ya Kilimo mjini Kisumu, Kenya, kiungo wake Kiggi Makassy atakwenda kutibiwa nchini India kufuatia kuumia katikati ya msimu uliopita akiichezea Simba SC mchezo wa kirafiki dhidi ya CDA mjini Dodoma.
    Taarifa ya Simba SC, imesema kwamba kwa sasa klabu hiyo inapanga ahadi na hospitali nchini India kwa ajili ya mchezaji huyo kwenda huko kutibiwa.
    Kiggi aliumia akiwa katika msimu wake wa kwanza tu tangu asajiliwe kutoka mahasimu, Yanga SC na jithada za kumponya kwa tiba za wataalamu wa nchini zimegonga mwamba na sasa anasogezwa mbele.
    Aidha, taarifa hiyo imesema kwamba, Simba SC inatarajia kuwa na wiki ya kijamii kuanzia Agosti 5 hadi 11, mwaka huu kuelekea tamasha la kuazimisha siku ya klabu ya klabu hiyo, maarufu kama Simba Day.
    Katika wiki hiyo, mabingwa hao wa zamani wa Bara watatembelea kituo cha watoto yatima na kuwafariji kwa misaada, watatembelea wagonjwa, watahudhuria kozi maalum iliyoandaliwa na wadhamini wao, Bia ya Kilimanjaro, watatembelea shule kuhamasisha watoto kupenda soka na hususan klabu hiyo ya Mtaa wa Msimbazi, watatembelea vyombo vya habari kuimarisha uhusiano na kufanya ibada maalum klabuni kwao, kuwarehemu wachezaji, viongzi, wanachama na wapenzi wa tmu hiyo waliotangulia mbele ya haki na kujiombea mema siku zijazo. 
    Katika hatua nyingine, Simba SC imesema Chuo Kikuu Huria kimekwishawakabidhi makabrasha ya awali ya Mpango Mkakati wa maendeleo ya klabu hiyo na Kamati ya Utendaji itakutana Julai 13 kuipitia, kabla ya kuirejesha kwa watalaamu wao hao ili ikamilishwe tayari kupelekwa kwenye Mkutano Mkuu wa wanachama kwa hatua zaidi.
    Simba pia itafanya ziara Katavi mkoani Rukwa, kwa mwaliko wa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  kucheza mechi ya kirafiki na itaondoka Dar es Salaam Julai 13 na baada ya hapo itaelekea kucheza mechi za kirafiki Tabora, Mwanza na Mara kabla ya kuweka kambi fupi Kenya na baadae kushiriki mashindano ya Kilimo yatakayofanyika Kisumu Kenya kuanzia Julai 31 hadi Agosti 4. 
    Wakati huo huo:  Simba B inatarajiwa kuondoka kesho Dar es Salaam  kwenda Arusha kwa ajili ya michuano ya Kombe la Rolingstone inayotarajiwa kuanza Julai 6, 2013.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: SIMBA SC KUSHIRIKI MASHINDANO YA KILIMO KENYA, KIGGI KUTIBIWA INDIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top