IMEWEKWA JULAI 22, 2013 SAA 7:51 USIKU
HAIJALISHI hata kama Wayne Rooney hatopatikana, inaonekana Fernando Torres atakabiliana na ushindani mkali kutoka kwa Romelu Lukaku.
Mshambuliaji huyo wa Ubelgiji anaendelea vizuri, akifunga kwa mara ya pili katika mechi mbili za kujiandaa na msimu, Chelsea ikiichapa Malaysia XI mabao 4-1 jana, na Jose Mourinho amesema hatahofia kuanza msimu na Lukaku akiongoza safu ya ushambuliaji.
"Ni hivyo," alisema Mourinho, alipoulizwa kama kweli atashindana na Torres na Demba Ba, ambaye alichukua nafasi ya Lukaku mapumziko mjini Kuala Lumpur.
Kiongozi wa safu ya ushambuliaji ajaye? Romelu Lukaku amemvutia Jose Mourinho katika mechi za Chelsea kujiandaa na msimu.
Lukaku anafanana mno kiuchezaji na shujaa wa zamani wa Chelsea, Didier Drogba awali Mourinho alipokuwa Chelsea, hivyo anamvutia sana kocha wake na anaweza kuongoza safu katika Ligi Kuu.
Torres hawezi kuwa na Mourinho tayari amekwishasema Mspanyola huyo aliyesajiliwa kwa Pauni Milioni 50 hana madhara anapibanwa na hakuna nafasi ya kushambulia nyuma ya mabeki.
Mfano wa kuigwa: Lukaku ni mshambuliaji hatari, kama alivyokuwa gwiji wa zamani wa Blues, Dider Drogba (kulia)
Mtu wa nguvu wa kuvutia: Jose Mourinho amefurahishwa na maendeleo ya Lukaku
Pamoja na hayo, Lukaku ana umri wa miaka 20 tu na Mourinho anaridhika kumbebesha mzigo huo tena kwa matarajio: "Tunatakiwa kumuheshimu Didier, kwa sababu ni wa kipekee katika historia ya Chelsea na tunatakiwa kumuheshimu Lukaku,"alisema kocha huyo.
"Kitu kizuri kufanya ni kwamba kutomfananisha na gwiji katika historia ya Chelsea. Muache Didier huko alipo, katika kiwango cha juu cha historia ya Chelsea, na muache Lukaku ajitume. Kijana ni mzuri,".
Ba ataanza Alhamisi katika mchezo wa mwisho wa ziara ya Asia dhidi ya Indonesia XI. Torres bado hajajiunga na kikosi akiendelea na mapumziko baada ya Kombe la Mabara.
Chelsea ilipata pigo la majeruhi pamoja na kushinda Malaysia, baada ya Kevin de Bruyne kutolewa nje kufuatia kuumia goti lake la kuli, akifunga bao la pili usiku huo.
De Bruyne, mwingine kati ya waliovutia katika ziara hiyo, aliondoka uwanjani akiwa ameshika mikono kichwani, ingawa taarifa za daktari zilisema hayatakuwa maumivu makubwa.
Ushindani: Kuchanganya kwa Lukaku ni habari mbaya kwa washambuliaji Demba Ba (kushoto) na Fernando Torres (kulia)
Bahati mbaya: Kiungo Mbelgiji, Kevin de Bruyne akitolewa nje baada ya kuumia
Lukaku akipongezwa na kinda wa miaka 17 aliye majaribio, Traore, ambaye ameng'ara Asia
Winga huyo Mbelgiji alifunga bao la kwanza kabla ya Bertrand Traore kufunga la pili, Lukaku la tatu na Victor Moses la nne, kabla ya Malaysia kupata la kufutia machozi.
Kiungo Traore ana miaka 17 tu na tayari ni mchezaji wa timu ya taifa ya Burkina Faso ambaye yupo kwenye majaribio kwa sababu ya viza ya mwanafunzi na hawezi kusaini Mkataba hadi atimize miaka 18 Septemba na hawezi kuomba kibali cha kufanya kazi.