IMEWEKWA JULAI 4, 2013 SAA 12: 28 ASUBUHI
MSHAMBULIAJI Wayne Rooney atatakiwa kuwasilisha barua ya maandishi ya kuomba kuondoka ikiwa anataka kuachana na Manchester United.
Mpachika mabao huyo wa Old Trafford, alirejea mazoezini jana huku mustakabali wake ukiwa bado haueleweki. Imefahamika hakuwa na Mkutano mahsusi na kocha mpya David Moyes juu ya suala lake.
Hilo linaweza kutokea katika kituo cha mazoezi cha klabu, Carrington leo. Wawili hao walizungumza jana, lakini si kwa muda mrefu na msimamo wa United kwake bado haujabadilika.
Hajielewi: Mustakabali wa Wayne Rooney bao haueleweki licha ya jana kurejea mazoezini
Wamesema mshambuliaji huyo wa England hauzwi. Kuhusu tetesi za wapinzani wao katika Ligi Kuu, Arsenal kutaka rasmi kumsajili tangu wiki iliyopita, United bado haijawasiliana na yoyote anayemtaka Rooney.
Sakata hili linaweza kugeuka tu iwapo mshambuliaji mwenyewe ataamua kulazimisha kuondoka. BIN ZUBEIRY iliandika mwishoni mwa msimu uliopita kwamba, Rooney aliomba kuondoka kwa kocha aliyestaafu, Sir Alex Ferguson.
Ombi la kuondoka litamaanisha Rooney hatadai chochote katika Mkataba wake wa miaka miwili uliobakia ambao alikuwa analipwa Pauni 250,000 kwa wiki.
Aliyepagawa: Mshambuliaji wa Manchester United hana furaha kwa sasa
Mabadikliko yote: David Moyes anaboresha benchi lake la Ufundi United
Anarudi Old Trafford? Phil Neville anaweza kuungana na Moyes Man United
Moyes, bado anataka kumuongeza katika benchi lake la ufundi, beki wa zamani wa United, Phil Neville na ni matumaini Rooney atakubali kubaki msimu ujao kufanya na kazi na kocha wa zamani wa Everton, aliyeinua kipaji chake Goodison Park.
Huku Moyes akitarajiwa kuzungumza na Waandishi wa Habari kwa mara ya kwanza kesho, ufafanuzi utakuja muda si mrefu.
Harudi: Angalau bado, kwa Cristiano Ronaldo
Wakati huo huo, mchezaji mwenzake wa zamani Rooney, Mreno Cristiano Ronaldo ameendelea kuweka wazi juu mapenzi yake na United. Mshambuliaji huyo wa Real Madrid amesema jana kwamba anataka kurudi Ligi Kuu, lakini hakusema lini.
"Nalikosa kweli soka la England. Kwangu ilikuwa moja ya miaka bora katika maisha yangu ya soka wakati nipo huko Manchester United. Ni klabu ambayo bado ipo moyoni mwangu. naikosa kweli kweli. Lakini kwa sasa maisha yangu yapo Hispania. Nafurahia kucheza huko pia. Mustakabali hatuwezi kuujua,"alisema Ronaldo.