IMEWEKWA JULAI 1, 2013 SAA 2:06 ASUBUHI
KOCHA David Moyes anajiandaa kukutana na Wayne Rooney na wawakilishi wake kwa mazungumzo kesho, hilo likiwa jukumu lake la kwanza kubwa tangu aanze kazi Manchester United.
Mkataba wa miaka sita wa Mscotland huyo umeanza rasmi leo na atakwenda makao makuu ya klabu, Carrington kutatua sakata la muda mrefu la Rooney kutaka kuondoka.
Moyes anataka Rooney abaki, lakini anafahamu mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 aliyesajiliwa kwa Pauni Milioni 25.6 mwaka 2004 anataka kuondoka.
Tingisha: Wayne Rooney alikuwa kwenye tamasha la muziki Glastonbury mwishoni mwa wiki
Chini ya utawala mpya: Moyes anashikilia mustakabali wa Rooney Old Trafford
Inafahamika mwanasoka huyo wa kimataifa wa England amejenga fikra zake kwamba kubadilisha klabu ni njia nzuri kufufua makali yake kuelekea Fainali za Kombe la Dunia majira yajayo ya joto.
Zaidi itategemea na mazungumzo yake na Moyes ambaye anafanya jitihada za kumbakiza.
Arsenal na Chelsea zote zinamfuatilia na zina ya kumsajili Rooney na ikiwa United itakubali kumuuza watalazimika kumuacha ajiunge na moja ya wapinzani wao katika Ligi Kuu England.
Kama Rooney atataka kuondoka, United pia inaweza ikataka ada ya uhamisho ya kiasi cha Pauni Milioni 35, ambazo Paris Saint-Germain na Real Madrid zinaweza kutoa kununua huduma ya mpachika mabao huyo.
Kocha wa Real, Carlo Ancelott ni shabiki wake, lakini kumfikiria Rooney itategemea na Mtaliano huyo mipango yake ya kuwasajili Luis Suarez wa Liverpool na Edinson Cavani wa Napoli itakuwaje.
Arsenal wako tayari kuvunja rekodi yao ya usajili na kumfanya pia Rooney awe mchezaji anayelipwa zaidi kwa kiasi cha mshahara wa Pauni 170,000 kwa wiki, ambacho ni cha chini kutoka Pauni 225,000 anazolipwa kwa sasa.
Moyes anatakiwa kumaliza suala hili mapema ikiwa anataka kumpata mbadala sahihi.
Aatashughulikia nyongeza ya dau la kutaka kumsajili beki wa kushoto wa Everton, Leighton Baines Pauni Milioni 15 na mazungumzo rasmi na Barcelona kuhusu usajili wa Pauni Milioni 17 wa kiungo Thiago Alcantara.
Mkataba mkubwa: Wayne Rooney atajadili mustakabali wake huku Arsenal na Chelsea zikimsikilizia
Bayern Munich, Manchester City na Real Madrid nazpo zinafuatilia pia sakata hilo. Monaco itamfuata Patrice Evra iwapo dili la Baines litakamilika na timu hiyo ya Ufaransa pia bado inamtaka winga Mreno wa United, Nani.
Kadhalika, suala la AC Milan kutaka kumsajili Nemanja Vidic limetupiliwa mbali na wakala wake, Silvano Martina aliyesema: "Vidic hana tatizo United, yanayozungumzwa yote ni uvumi,".
Wakati huo huo, Arsenal ofa yake ya Pauni Milioni 6 kwa kiungo wa Lyon, Clement Grenier, mwenye umri wa miaka 22 imepigwa chini.