IMEWEKWA JULAI 2, 2013 SAA 2:39 USIKU
KLABU za Chelsea na Manchester City zitalazimika kuvunja rekodi ya dau la usajili Uingereza kama zinataka kumsaini mshambuliaji wa Napoli, Edinson Cavani baada ya matajiri wa Ufaransa, Paris Saint-Germain kutoa ofa ya Pauni Milioni 43 kwa nyota huyo wa Uruguay.
Cavani anatakiwa na klabu zote, Chelsea na City, lakini dau la PSG linamaanisha watatakiwa kupanda ili kilipiku ndipo wampate mshambuliaji huyo.
Dau la PSG linakaribia Pauni Milioni 53.9, ambazo Napoli inataka ambazo zitahusu pia kodi wa dili hilo.
Kifaa: Edinson Cavani alifunga mabao mawili dhidi ya Italia waakti Uruguay ikifungwa kwa penalti mechi ya mshindi wa tatu Kombe la Mabara.
Real Madrid bado haijafika bei na Cavani alisema wiki iliyopita kwamba tetesi zimezidi kuhusu hatima yake.
"Mwanzoni mwa Kombe la Mabara, sikuamini kwamba tetesi za usajili zingenisababishia matatizo. Lakini, mwishoni, nakubali wananisumbua kidogo,"alisema.
Chelsea inashikilia rekodi ya kusajili kwa bei chafu Uingereza, Pauni Milioni 50 walizotoa kumsaini Fernando Torres, Januari 2011.
VIDEO: Angalia bao la kwanza la Cavani dhidi ya Italia Kombe la Mabara
Na la pili (hili ni tamu zaidi )