IMEWEKWA JULAI 2, 2013 SAA 11:54 ALFAJIRI
KLABU ya Tottenham imeshinda mbio za kuwania saini ya kiungo Mbrazil, Paulinho baada ya kuthibitisha atajiunga na timu hiyo kwa ada ya uhamisho ya Pauni Milioni 17.
Mchezaji huyo kwa kiasi kikubwa alitarajiwa kuondoka klabu ya Brazil kutua England baada ya Fainali ya Kombe la Mabara Jumapili kama ilivyowahi kuandika BIN ZUBEIRY.
Na katika Mkutano na Waandishi wa Habari, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 alijikuta akilia wakati anaelezea uhamisho huo.
Hisia: Paulinho akimwaga machozi katika Mkutano na Waandishi wa Habari, Corinthians kutangaza kuhamia kwake Tottenham
"Ni vigumu kusema chochote mapema namna hii, lakini uhakika hiyo ilikuwa miaka ya ajabu katika maisha yangu ya soka, na mataji mengi,"alisema.
"Kitu nachopenda kusema kwa mashabiki wa Corinthians, bodi na viongozi ni! Tutaona muda mfupi! - Nitarudi katika wakati usiojulikana, kutokana na yote waliyonifanyia.
"Mataji yangu binafsi yote ni shukrani kwa klabu, Corinthians itabakia moyoni mwangu katika wote wa maisha yangu,".
Mkurugenzi wa Soka wa Corinthians, Roberto de Andrade amemsifu mchezaji huyo aliyeng'ara katika kikosi ch Brazil kilichoifunga Hispania 3-0 mjini Rio Jumapili.
Amesaini: Paulinho ameisaidia Brazil kutwaa Kombe la Mabara kwa kuifunga Hispania 3-0 kwenye Fainali
"Nataka kumshukuru Paulinhokwa kila kitu alichoifanyia Corinthians,"alisema.
"Hatutamsahau - jinsi alivyo mtu babu kubwa - na taji la timu yake ya taifa (Kombe la Mabara aliloshinda na Brazil) ilistahili.
"Corinthians inajivunia kuwa na mchezaji kama yeye. Ni halali kuhamishia masha yake katika klabu ya English, kujua utamadunia mpya.".