IMEWEKWA JULAI 4, 2013 SAA 3:28 ASUBUHI
KLABU ya Manchester City inataka kumsajili mshambuliaji anayeuzwa Pauni Milioni 18 wa Sevilla, Alvaro Negredo.
Majadiliano hayajaanza, lakini kocha Manuel Pellegrini amemtambulisha mshambuliaji huyo wa Hispania kama mtu anayemhitaji kuziba pengo la Carlos Tevez.
Pellegrini alijaribu kumsaini Negredo wakati akiikochi Malaga, lakini sasa kutokana na uhusiano mzuri baina ya City na Sevilla unaotokana na Mkurugenzi wa Soka, Txiki Begiristain na usajili wa Jesus Navas, kocha huyo wa City anataka kujaribu tena.
Anatakiwa: Alvaro Negredo ametajwa katika orodha ya wanaotakiwa na Manchester City kwa Pauni Milioni 18
Kuingia kwa mwongozo sahihi: Manuel Pellegrini anatazamiwa kuingiza sura mpya Manchester City
Negredo, mwenye umri wa miaka 27, alitarajiwa kusaini Atletico Madrid wiki hii, lakini dili hilo lilishindikana kutokana na ada kubwa iliyotakiwa na Sevilla, Pauni Milioni 21.2kwa wapinzani wao hao wa La Liga.
Rais Jose Maria del Nido alionekana wazi kutotataka kumuuza mchezaji huyo, lakini ilikuwa kabla ya kuibuka kwa ofa kutoka England.
Kocha wa City pia anamtaka mshambuliaji wa Benfica, Oscar Cardozo na wa Bayern Munich, Mario Gomez ambaye yupo kwenye mazungumzo na Fiorentina.
Amejiunga na klabu: Manchester City tayari imemsaini Jesus Navas kutoka Sevilla majira haya ya joto
Changamoto mpya: Carlos Tevez ameondoka City na kutua Juventus