IMEWEKWA JULAI 24, 2013 SAA 3:54 USIKU
HAUKUWA mwanzo mzuri wa maisha ya kocha Manuel Pellegrini katika soka ya England, lakini leo amepata ushindi wa kwanza Manchester City ikishinda 1-0 dhidi ya China Kusini, bao pekee la Edin Dzeko dakika ya 21.
Vipigo viwili Afrika Kusini katika mechi za mwanzo za Manchester City kujiandaa na msimu na kifo cha mama yake mkubwa, Silvia, ambacho kilimrejesha ghafla nyumbani Chile ndani ya mwezi mmoja tangu aanze kazi.
Ilitarajiwa Pellegrini angekaa Santiago kwa zaidi, lakini amerejea kazini haraka katika ziara ya Kombe la Barclays Asia na kutua Hong Kong saa 24 baada ya mazishi.
Kikosi cha Man City kilikuwa: Hart, Zabaleta/Sinclair dk75, Kompany, Lescott, Clichy/Kolarov dk45, Milner, Nasri, Barry/Rodwell dk55, Fernandinho/Javi Garcia dk65, Toure/Negredo dk55 na Dzeko/Richards dk75.
China Kusini: Barry, Chak, Ticao, Cheng/Martins dk45, Naves, Lee Wai Lim/Lee Hong Lim dk52, Sealy, Tse, Joel, Kwok na Zhang.
Bao: Edin Dzeko akifunga bao la ushindi dakika ya 21 kwa kichwa akiunganisha krosi ya James Milner
Kwok Kin Pong wa China Kusini akipiga kichwa mpira dhiai ya James Milner
Amerudi kazini: Pellegrini amerejea kazini baada ya mazishi ya mama yake mkubwa
Kivutio: Negredo (kushoto) aling'ara leo akitokea benchi kama anavyoonekana akimtoka Kolarov (kulia)
Mikono salama: Hart aliokoa vizuri leo
Mlinzi: Kompany akimkimbiza mshambuliaji wa China Kusini
Nyomi ya mashabiki