IMEWEKWA JULAI 4, 2013 SAA 6:10 MCHANA
Ndege Watatu: Kutoka kushoto ni Paulyne Zongo, Khadija Mnoga (Kimobitel) na Joan Matovolwa, wanamuziki hao watatu wa kike na wakongwe nchini wameanzisha kundi lao litakalojulikana kwa jina la Ndege Watatu, ambalo litakuwa likifanya vitu vyake muda si mrefu kuanzi sasa nchini.
Kundi la Ndege 3 linaloundwa na wanamuziki wakongwe katika Tasnia ya muziki wa dansi na kizazi kipya Joan matovolwa, Khadija Mnoga (Kimobitel) na Paulyne Zongo, hivi karibuni limeshatoa kibao chake kinachokwenda kwa jina la Misukosuko ya Mapenzi, ambacho kimekwishaanza kuchezwa katika stesheni mbalimbali za Redio nchini.
Misukosuko ya Mapenzi ni wimbo ambao imetungwa kwa umahiri wa hali ya juu, na kuonyesha viwango vya juu katika uimbaji na utunzi.
Kwa sasa Joan Matovolwa na Paulyne Zongo ni wanamuziki huru, wakati Khadija Mnoga 'Kimobitel' anaimbia bendi ya Extra Bongo inayoongozwa na Ally Choki.