IMEWEKWA JULAI 3, 2013 SAA 5:27 ASUBUHI
MBRAZIL Neymar na Muargentina, Lionel Messi wataunda pamoja safu kali ya ushambuliaji ya Barcelona msimu ujao, lakini walikuwa timu tofauti leo katika mechi ya Hisani nchini Peru.
Nyota hao wa Amerika Kusini, waliungana na wakali kama Daniel Alves, Ezequiel Lavezzi, Javier Mascherano na Eric Abidal kwa mechi hiyo baina ya Messi na marafiki zake dhidi ya wachezaji wengine duniani.
Karibu sana: Lionel Messi (kulia) na Neymar
Vijana wa Barca: Lakini Neymar na Messi walikuwa timu tofauti katika mechi hiyo ya hisani
Video: Neymar afunga kwa umbali wa mita 45
Ilikuwa mara ya kwanza wanakutana uwanjani tangu gwiji wa Barca, Johan Cruyff ashauri mshindi mara nne wa Balon D'or, Messi auzwe kumuachia nafasi mchezaji mwenzake mpya aliyesajiliwa kwa Pauni Milioni 50.
Na Neymar alimgaragaza Messi, ambao wote walivaa jezi namba 10 katika mechi hiyo, kwa kufunga bao la umbali wa mita 45.
Na baadaye akamnyanyasa beki wa Malaga na Uruguay, Diego Lugano.
Lakini Messi ndiye aliyeibuka kifua mbele mwishowe kwa timu yake kushinda 8-5.
Fedha zote zitakazopatikana katika mchezo huo, zitakwenda kwenye mfuko wa kujenga mustakabali mzuri wa maisha kwa watoto kimataifa.
Mwenye mpira: Neymar, kushoto, akimtoka Muargentina, Javier Mascherano, kulia,
Mtu wa mbele: Lionel Messi, kushoto, ameandaa mechi ya Hisani Peru
Marafiki wameungana: Messi na Daniel Alves, Ezequiel Lavezzi na Eric Abidal
Nyomi: Mashabiki wakimpiga picha Messi
Cheki vitu: Neymar akimnyanyasa Diego Lugano wa Uruguay
Mburudishaji: Neymar akichezea mpira kwa kichwa chake
Video: Neymar akimfanya kitu mbaya Lugano