IMEWEKWA JULAI 4, 2013 SAA 6:25 MCHANA
KIUNGO wa Vitesse Arnhem, Marco van Ginkel anajiandaa kukamilisha uhamisho wa kutua Chelsea, baada ya klabu hizo kukubaliana biashara ya Pauni Milioni 9.
Van Ginkel, mwenye umri wa miaka 20, ambaye amiechezea mechi moja Uholanzi, sasa anatakiwa tu kufuzu vipimo vya afya na kukubali maslahi binafsi aliyopangiwa ili kuwa mchezaji wa pili kusainiwa na Jose Mourinho baada ya Andre Schurrle.
Taarifa katika tovuti ya Chelsea imesomeka: "Chelsea FC na Vitesse Arnhem zimefikia makubaliano ya uhamisho wa Marco van Ginkel.
Mholanzi kiwango: Kiungo Marco van Ginkel (kulia) anajiandaa kuhamia Chelsea akitokea Vitesse Arnhem
"Mchezaji huyo atajiunga na Chelsea baada ya kufuzu vipimo vya afya, makubalino ya maslahi yake binafsi na masuala ya kisheria,".
Van Ginkel alijiunga Vitesse akiwa na umri wa miaka saba mwaka 1999 na kuendelea kukuzwa katika programu ya vijana, kabla ya kuanza kukomazwa timu ya wakubwa mwaka 2010.
Amechezea vikosi vya vijana vya Uholanzi chini ya miaka 19 na 21 na aliichezea kwa mara ya kwanza timu ya wakubwa ya nchi hiyo katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Ujerumani mwaka jana.
Uhamisho huo utamfanya Mourinho awe ametumia jumla ya kiasi cha Pauni Milioni 27 hadi sasa tangu amerejea kupiga kazi Stamford Bridge kwa mara ya pili, baada ya awali kumsajili mshambuliaji wa Kijerumani, Schurrle kutoka Bayer Leverkusen kwa mkataba wa miaka mitano.
Amesajiliwa: Andre Schurrle amemwaga wino miaka mitano na kupewa jezi namba 14
VIDEO: Bao tamu alilofunga Van Ginkel msimu uliopita