IMEWEKWA JULAI 28, 2013 SAA 9:03 ALASIRI
BONDIA maarufu wa Filipino, Manny Pacquiao amesema kwamba anataka kugombea Urais wa nchi hiyos atakapotungika glavu zake.
Mwanamasumbwi huyo mwenye umri wa miaka 34 amekuwa kwenye siasa kwa miaka kadhaa sasa, tangu achaguliwe kwenye Bunge la nchi hiyo mwaka 2007.
Akizungumza na AFP, Pacquiao amesema: "Wakati naanza ngumi, kwa sababu nilipanga, unajua nilifikiria kuwa bingwa. Hivyo wakati naingia kwenye siasa, ni kitu kile kile,".
Atakuwa Rais? Bondia wa Filipino na Mbunge wa Sarangani, Manny Pacquiao
Anarudi ulingoni: Pambano lijalo la Pacquiao ni dhidi ya Mmarekani, Brandon Rios mwezi Novemba
Pacquiao amekuwa bingwa wa dunia katika madaraja nane ya uzito tofauti, na kwa sasa ni Mbunge wa Sarangani nchini humo.
Pambano lake lijalo atapigana na Brandon Rios wa Marekani, November 24 likiwa pambano la kwanza tangu apigwe na Juan Manuel Marquez, hilo likiwa pambano la tano kupoteza katika historia yake.
Sura maarufu: George Foreman alikuwepo katika Mkutano na Waandishi wa Habari kutangaza pambano la Pacquiao na Rios
Akizungumzia pambano lake lijalo na Rios, alisema: "Yuko sawa, lakini naweza kusema ni mpiganaji mzuri na anapenda kupigana kwa karibu, anapenda gumba kwa gumba(kidole).
"Hili litakuwa pambano zuri-- matukio zaidi ulingoni. Ni matumani yangu hatakimbia,".
Pacquiao kwa sasa ni Mbunge Sarangani na anataka Urais