IMEWEKWA JULAI 19, 2013 SAA 6:00 USIKU
BILA kocha hakuna ushindi hapa Afrika Kusini, Manchester City imemaliza mzunguko wa kwanza wa ziara yake ya kujiandaa na msimu kwa maumivu mjini Durban.
BILA kocha hakuna ushindi hapa Afrika Kusini, Manchester City imemaliza mzunguko wa kwanza wa ziara yake ya kujiandaa na msimu kwa maumivu mjini Durban.
Kuondoka ghafa kwa kocha Manuel Pellegrini na kutowasili kwa Alvaro Negredo na Stevan Jovetic kumeifanya City ifungwe kwenye Uwanja wa Moses Mabidha kwa bao la dakika za lala salama la penalti.
Kilikuwa kipigo cha pili baada ya Jumapili kuchapwa mabao 2-0 na SuperSport mjini Pretoria, kocha Pellegrini akiukosa mchezo huo baada ya kusafiri ghafla kurejea nyumbani kwao Chile kwa sababu za kifamilia.
La kwanza: Bongani Ndulula wa AmaZulu akifunga bao la kwanza katika ushindi wa 2-1 dhidi ya Manchester City
Kocha huyo mpya alipanga kikosi cha kucheza mechi hiyo kabla ya kuondoka kwenda Santiago, akimuanzisha mchezaji mpya aliyesajiliwa kwa Pauni Milioni 30, Fernandinho sambamba na Yaya Toure katika safu ya kiungo kwa mara ya kwanza.
Wachezaji wa Pellegrini bado wanachanganya taratibu baada ya kurejea mazoezini kiasi kama cha wiki mbili kutoka mapumzikoni na David Silva na mchezaji mpya, Jesus Navas – ambaye ataungana na Negredo na Jovetic hawajaripoti.
La kusawazisha: James Milner aliisawazishia Manchester City
Ameondoka: Manuel Pellegrini amerejea nyumbani Chile kwa matatizo binafsi
Mabao ya Amazulu yalifungwa na Ndulula dakika ya 20 na Van Heerden kwa penalti dakika ya 87, wakati la City lilifungwa na Milner dakika ya 26.
Mabao ya Amazulu yalifungwa na Ndulula dakika ya 20 na Van Heerden kwa penalti dakika ya 87, wakati la City lilifungwa na Milner dakika ya 26.
Kikosi cha Amazulu kilikuwa: Kapini; Macala, Teyise, Msekeli, Hlanti; Madondo, Madubanya, Manqana, Zondi, Dlamini; Ndulula.
Man City: Hart/Pantilimon dk63, Richards/Zabaleta dk46, Kompany/Garcia dk46, Nastasic/Lescott dk69, Kolarov/Boyata dk75, Milner/Razak dk75, Toure/Rodwell dk46, Fernandinho/Barry dk69, Sinclair, Dzeko/Nimely dk75 na Nasri/Suarez dk69.
Mashabiki: Mashabiki wa Afrika Kusini wakiisapoti Man City
Nahodha wa City, Vincent Kompany akimiliki mpira
Edin Dzeko akijaribu kupasua ukuta wa Amazulu
Samir Nasri akiambaa na mpira