IMEWEKWA JULAI 31, 2013 SAA 4:11 USIKU
MANENO ya kocha Manuel Pellegrini kwamba ana safu kali ya ushambuliaji dunia nzima, yameanza kudhihirika taratibu baada ya timu yake, Manchester City kuvuna mvua ya mabao kwenye mechi ya Kombe la Audi leo Uwanja wa Allianz Arena mjini Munich.
Mabao matano ndani ya dakika 35, yameitotesha AC Milan iliyopambana na kurudisha hadi kulala kwa 5-3.
David Silva alifunga bao la kwanza dakika ya tatu, kufuatia kazi nzuri ya Stevan Jovetic, na Micah Richards na Aleksandar Kolarov wakaongeza mengine dakika ya 19 na 22 na Edin Dzeko akafunga mawili ndani ya dakika tatu.
Stephan El Shaarawy akafunga mawili na Andrea Petagna akafunga lingine katika mabao matatu ya Milan.
Kapu la mabao: Manchester City imefiunga AC Milan 5-3 katika Nusu Fainali ya Kombe la Audi
David Silva (kulia) aliifungia la kwanza Manchester City
Micah Richards akifunga la pili
Delight: Richards celebrates his goal with new signing Fernandinho at the Allianz Arena
Aleksandar Kolarov akiwafungia Manchester City la tatu
Kolarov na Richards wakishangilia
Edin Dzeko alihitimisha karamu ya mabao ya City
Ametulia: Manuel Pellegrini akiangalia mechi
Hana furaha: kipa Marco Amelia akionekana aliyeudhika
Stephan El Shaarawy alifunga mawili kwa Milan
Andrea Petagna alimtungua bao zuri Joe Hart dakika ya 43