IMEWEKWA JULAI 21, 2013 SAA 2:37 USIKU
KOCHA Arsene Wenger amepata pigo tena katika safu yake ya ulinzi leo, baada ya Laurent Koscielny kugongana na kipa Wojciech Szczesny mazoezini na kuumia, hivyo ataukosa mchezo wa kirafiki kesho mjini Nagoya.
Beki Mfaransa, Koscielny alitoka kwenye mazoezi mwishoni akionekana kama aliyeumia kifundo cha mguu wa kulia.
Mara moja alitazamwa na dawati la tiba la The Gunners juu ya maumivu yake, kabla ya kupelekwa Uwanja wa Rugby wa Mizuno kwa uchunguzi zaidi.
Laurent Koscielny alikuwa na morali ya hali ya juu katika mazoezi ya leo kabla ya kuumia
Theo Walcott akisaini autographs kwa mashabiki Nagoya
Arsene Wenger akizungumza na mashabiki wakati wa mazoezi
Ukubwa wa maumivu yaked bado haujajulikana, lakini anaonekana hatacheza mechi ya kesho.
Benchi la Ufundi la Arsenal litafuatilia tatizo kwa saa 24, lakini wanaamini halitakuwa tatizo la muda mrefu.
Na katika pigo lingine, Szczesny naye anaweza kuukosa mchezo wa kesho kutokana na maumivu.
Walinzi wakiwadhibiti mashabiki waliokuwa wanasubiri nyota wa Arsenal wawasili
Saini hapa: Bacary Sagna akipasua katika ya umri ya mashabiki wakati Arsenal inakwenda kufanya mazoezi
Kikosi cha TArsenal kikipasha nchini Japan
Furaha kuwa hapa: Wachezaji wa England, Alex Oxlade-Chamberlain na Theo Walcott wakipozi kwa picha wakati wa mazoezi
Mpland huyo inafahamika aliumia mazoezini tangu wawasili Japan Ijumaa asubuhi.
Aisha, Lukasz Fabianski au Damien Martinez mmojawapo atachukua nafasi ya Szczesny dhidi ya Nagoya Grampus.
Habari za kuumia kwa Koscielny zinamaanisha Wenger ambaye kwa sasa tayari anamkosa beki wake mmoja mzoefu, Per Mertesacker katika ziara hii ya Mashariki ya Mbali; atamtumia kinda Ignasi Miquel kikosini.
Wenger tayari anamkosa Thomas Vermaelen, ambaye yuko nje kwa miezi mitatu kwa majeruhi.
Walcott akisaini autographs kabla ya kuingia mazoezini
Lukas Podolski akipozi kwa ajili ya kamera akiwa ndani ya basi la timu
Mpiga picha: Podolski aligeuka mpiga picha wakati wa mazoezi Japan
Per Mertesacker mazoezini Japan
Maumivu ya Koscielny yanaweza kumfanya Wenger aharakishe jitihada za kumsajili sentahafu wa Swansea, Ashley Williams anayemuwania kwa muda mrefu.
Mshambuliaji Olivier Giroud, ambaye ni mfungaji bora wa klabu katika mechi hizi za kujiandaa na msimu, akifunga mabao matano katika mechi mbili, pia aliumia mazoezini, lakini akainuka na kuendelea.