IMEWEKWA JULAI 23, 2013 SAA 12:14 JIONI
MAISHA si mepesi kwa David Moyes bara la Asia. Siyo tu kocha huyo mpya wa Manchester United anavyosotea saini ya kiungo wa Barcelona, Cesc Fabregas, timu yake sasa imepoteza mechi ya pili kati ya tatu za ziara ya kujiandaa na msimu.
Mchezo huo ulikuwa mgumu kuliko wa Jumamosi dhidi ya A-League All-Stars mjini Sydney na Manchester United imefungwa mabao 3-2 na Yokohama nchini Japan.
Baada ya kutanguliwa kwa bao la mapema sekunde ya 27, United ilipigana kiume na kufanikiwa kuongoza kwa mabao 2-1 hadi mapumziko baada ya Jess Lingard kusawazisha dakika ya 19 na beki wa Marinos, Masakazu Tashiro kujifunga dakika ya 31.
Marquinhos akifunga bao la kwanza sekunde ya 27
Jesse Lingard (kulia) amekuwa katika kiwango kizuri na ameifungia bao United leo
Kikosi cha Man United kilikuwa: De Gea; Fabio, Jones, Evans/Smalling, Evra, Anderson, Cleverley, Zaha/Giggs, Lingard/Ashley Young, Januzaj/Kagawa na Van Persie/Welbeck.Lakini timu ya Japanese ikasawazisha haraka kipindi cha pili na ikapata bao la ushindi zikiwa zimesalia dakika tatu, wakati Yoshihito Fujita aliyetokea benchi alipomtungua David de Gea kutoka umbali wa mita 12, baada ya Jin Hanato kuwatoka Patrice Evra na Phil Jones upande wa kushoto.
Yokohama: Enomoto, Dutra, Aguiar, Tashiro, Kobayahsi, Nakamura, Hyodo, Tomisawa, Nakamachi, Marquinhos na Sato.
Robin van Persie akijaribu kumtoka beki wa Yokohama Marinos, Masakazu Tashiro
Van Persie akipiga mpira mbele ya beki wa Kijapan, Yuzo Kobayashi
Kinda wa United, Adnan Januzaj akigombea mpira na Dutra
Mashabiki wawili wa wakimsapoti Shinji Kagawa na Robin van Persie
Wilfried Zaha yuko vizuri
Shinji Kagawa alikuwa kivutio
David Moyes akimuangalia Danny Welbeck akirusha mpira
Lingard akifunga badaa ya kazi nzuri ya Wilfried Zaha
Shinji Kagawa (kushoto) aling'ara akicheza nyumbani
Danny Welbeck akipambana
Wajeshi Wekundu: Mashabiki watoto wa United
Mashabiki wa Japan wakiwa wamevaa jezi ya nyota wa United, Kagawa
Nyota wa Japan, Kagawa anapendwa mno nyumbani