Na Mahmoud Zubeiry, IMEWEKWA JULAI 19, 2013 SAA 5:20 USIKU
KIUNGO wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Shomary Kapombe ameondoka usiku huu Dar es Salaam kwenda Uholanzi kufanya majaribio ya kucheza soka ya kulipwa nchini humo.
Ameondoka na ndege ya KLM saa 5:30 usiku.
Akizungumza na BIN ZUBEIRY Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere usiku huu kabla ya kuondoka, Kapombe amesema kwamba anaondoka akiwa fiti, hana maumivu na yupo katika hali nzuri kimchezo, hivyo anaomba Mungu akamsaidie kufanya vizuri huko.
“Bado sijajua haswa programu yangu huko itakuwaje, nitakapofika ndio wakala wangu atanipa kila kitu kuhusu ratiba ya huko na nipo tayari kukabiliana na changamoto zozote,”alisema Kapombe.
Kiungo huyo ambaye kwa siku za karibuni amekuwa akitumiwa katika nafasi za ulinzi zaidi, beki pembeni na kati, amesema anakwenda Uholanzi kujaribu bahati yake na atakubaliana na hali yoyote, hata akifeli atarudi nyumbani kujipanga upya.
“Wakati mwingine katika maisha unahitaji bahati pia. Ila, niko sawasawa ile mbaya, kama Mungu kaniandikia nicheza Ulaya nitacheza tu, lakini mimi nakuhakikishia hiyo ndiyo nia yangu,”alisema.
Kapombe amelazimika kuiacha kambi ya Stars mjini Mwanza inayojiandaa na mchezo wa marudiano dhidi ya Uganda wikiendi ijayo mjini Kampala, kuwania tiketi ya kucheza Fainali za CHAN mwakani kwa ajili ya safari hiyo.
Stars inaendelea na mazoezi mjini Mwanza na kocha Kim Poulsen pamoja na kutoa ruhusa Kapombe aende Uholanzi, lakini hajaita mtu wa kuziba pengo lake.
Tayari kiungo wa Simba SC, Mwinyi Kazimoto ametoroka kwenye kambi hiyo na inadaiwa amekwenda Qatar kutafuta timu, lakini huyo pengo lake limezibwa na Mudathir Yahya wa Azam FC.
Kila la heri Shomary Kapombe. Mungu akujaalie ufanikiwe.

Amepaa; Kapombe ameondoka usiku huu kwenda Uholanzi |

Wa Qatar; Mwinyi kazimoto amekwenda Qatar, lakini hakuaga |