// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); DROGBA KUMBE 'DHULUMATI', MAHAKAMA YAMKUTA NA HATIA NA KUMUAMURU ALIPE EURO 450,000 - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE DROGBA KUMBE 'DHULUMATI', MAHAKAMA YAMKUTA NA HATIA NA KUMUAMURU ALIPE EURO 450,000 - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Tuesday, July 02, 2013

    DROGBA KUMBE 'DHULUMATI', MAHAKAMA YAMKUTA NA HATIA NA KUMUAMURU ALIPE EURO 450,000

    Didier Drogba
    IMEWEKWA JULAI 2, 2013 SAA 5:19 ASUBUHI

    MAHAKAMA Ufaransa imemuagiza mwanasoka wa kimataifa wa Ivory Coast, Didier Drogba kulipa Euro 450,000 kwa kampuni ya ujenzi ya mjini Corsica baada ya kutoilipa kwa kumfanyia kazi mjini mjini Abidjan.
    Kampuni ya Acqua Viva ilimfikisha kortini mshambuliaji huyo wa zamani wa Chelsea Mei kwa kugoma kulipa salio la malipo baada ya kujengewa nyumba ya kifahari iliyokamilika mwaka 2009.
    Kampuni hiyo imelalamika pia wafanyakazi wake kuzuiwa kufika eneo la nyumba hiyo waliyojenga, kitu ambacho Jaji amesema si haki na kwamba kilitokana na maelekezo ya Drogba na mkewe, raia wa Mali, Lala Diakite.
    Wakati mchezaji huyo wa zamani wa Marseille mwenye umri wa miaka 35, aliyejiunga na Galatasaray ya Uturuki mapema mwaka huu, ameamua kukata rufaa, lazima alipe fedha hizo mapema ili kutekeleza amri ya Mahakama.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: DROGBA KUMBE 'DHULUMATI', MAHAKAMA YAMKUTA NA HATIA NA KUMUAMURU ALIPE EURO 450,000 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top