IMEWEKWA JULAI 3, 2013 SAA 12:56 ASUBUHI
KLABU ya Chelsea itaanza rasmi harakati za kuwasajili Wayne Rooney na Robert Lewandowski baada ya Paris Saint-Germain kuweka mezani dau la Pauni Milioni 43 kwa ajili ya mshambuliaji wa Napoli, Edinson Cavani jana.
Roman Abramovich hataki kuingia kwenye vita ya kumgombea Cavani anayetakiwa sana na klabu yake, ingawa pia dau lililotolewa na mabingwa hao wa Ufaransa, wanaomilikiwa na mabilionea wa Qatari, ni pungufu ya Pauni Milioni 11 kutoka kiasi anachouzwa nyota huyo wa Uruguay.
Abramovich alivunja rekodi ya usajili Uingereza alipoilipa Liverpool Pauni Milioni 50 kumnunua Fernando Torres Januari mwaka 2011 na ingawa amepania kumpa sapoti Jose Mourinho katika soko la usajili anahofia kuingia hasara nyingine kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26.
Anaikubali bluu? Wayne Rooney sasa ndiye mshambuliaji mkuu anayewania na Chelsea baada ya bei Edinson Cavani kupanda
Mimi pia: The Blues pia wameelekeza ndoana zao kwa mapchika mabao wa Borussia Dortmund, Robert Lewandowski
Torres alikuwa pia ana umri wa miaka 26 wakati anawasili na thamani yake imeshuka sana baada ya hapo.
Mshahara si kitu: Chelsea inaweza kumlipa Cavani Pauni 250,000 kwa wiki alizotaka, lakini kama Rooney na Lewandowski watapatikana kwa bei rahisi hata kila mmoja akija na yake, itakuwa bora.
Katika kesi ya Rooney, Manchester United haitataka nkuwaongezea nguvu wapinzani wao kwenye mbio za ubingwa, wakati Lewandowski wazi anataka kuondoka Borussia Dortmund na alitaka kujiunga na Bayern Munich.
Anatakiwa: Edinson Cavani ametengewa dau kubwa na PSG, ambalo linaifanya Chelsea ijitoea kuwania saini yake
Amerejea: Roman Abramovich bado anataka kumsaidia Jose Mourinho katika soko la usajili
Manchester City, ambayo mshambuliaji wake, Edin Dzeko anaweza kuwa kwenye rada za Chelsea, imekuwa ikimfuatilia Cavani kwa muda mrefu, lakini sasa watalazimika kupanda dau kulipiku la PSG.
Real Madrid inatarajiwa kuwa klabu mpya ya Cavani ikiwa ataondoka Napoli, huku timu hiyo ya Hispania pia ikimtaka na mchezaji mwenzake wa timu ya taifa ya Uruguay, Luis Suarez.
Rooney anatarajiwa kuwa na kikao na kocha mpya wa United, David Moyes juu ya mustakabali wake kabla ya kikosi kwenda kwenye ziara ya kujiandaa na msimu mpya Asia na Australia wiki zijazo.
Nafasi kwa Real: Real Madrid, na kocha wake mpya, Carlo Ancelotti, inabakia chaguo la kwanza kwa Cavani
Muuaji: Cavani alifunga mabao mawili Uruguay ikitoka 2-2 na Italia katika mechi ya kusaka mshindi wa tatu Kombe la Mabara, kabla ya kufungwa kwa matuta