Shughuli imekamilika: Wachezaji wa Brazil wakiinua Kombe la Mabara baada ya kuwafunga mabingwa wa dunia, Hispania
Sema hureee: David Luiz akiwa na Kombe baada ya sherehe Maracana
Nyota wa mchezo: Neymar ameanza kupata mafanikio kimataifa
Mwimbaji wa Colombia, Shakira alikuwepo Rio kumuangalia mpenzi wake, Gerard Pique akiichezea Hispania
IMEWEKWA JULAI 1, 2013 SAA 9:05 USIKU
BRAZIL imetwaa Kombe la Mabara baada ya kuifunha Hispania mabao 3-0 kwenye Uwanja wa Jornalista Mario Filho (Maracana) mjini Rio de Janeiro, Brazil.
Katika mchezo huo, mabingwa wa Dunia na Ulaya walipoteza mchezaji mmoja na pia wakashindwa kufunga kwa penalti.
Shukrani kwao Fred aliyefunga mawili, la kwanza dakika ya pili na la tatu dakika ya 47 kwa pasi ya Hulk na Neymar aliyefunga la pili dakika ya 44 kwa pasi ya Oscar.
Dakika ya 68, Pique alitolewa nje kwa kadi nyekundu kwa kumchezea rafu mchezaji mwenzake mpya wa Barcelona, Neymar.
Dakika ya 54 Marcelo alimuangusha kwenye eneo la hatari Navas, lakini Sergio Ramos akakosa penalti baada ya mkwaju wake kuota mbawa.
Kikosi cha Brazil kilikuwa: Julio Cesar; Dani Alves, Thiago Silva (capt), David Luiz, Marcelo; Oscar, Luiz Gustavo, Paulinho/Hernanes dk 88; Fred/Jo dk80, Neymar, Hulk/Jadson dk73.
Hispania: Iker Casillas; Alvaro Arbeloa/Azpilicueta dk46, Gerard Pique, Sergio Ramos, Jordi Alba; Xavi, Sergio Busquets, Andres Iniesta; Juan Mata/Navas dk 52, Fernando Torres/Villa dk 59 na Pedro.
Mkombozi: Fred amefunga mawili
Pata picha itakuwaje Lionel Messi atakapoanza kucheza pamoja na Neymar
Kwaheri: Gerard Pique akionyeshwa kadi nyekundu baada ya kumuumiza Neymar aliyelala chini
Penalti ya Sergio Ramos iliota mbawa
Mechi imaisha? Fred akishangilia bao lake la pili na la tatu kwa Brazil
Kazi ya ziada: David Luiz aliokoa kwenye mstari wa goli shuti la Pedro, ambalo kama lingeingia ingekuwa 2-1
Neymar akifumua kumtungua Iker Casillas na kufanya 2-0
Shangwe tu: Neymar akiwarukia mashabiki Maracana
Kijana mwenye bahati: Alvaro Arbeloa angepewa kadi nyekundu kwa rafu aliyomchezea Neymar - wachezaji hao walikuwa peke yao wakati wa mapumzi beki huyo wa Real Madrid alipomuangusha mwenzake
FFU wa Brazil: Polisi wa kutuliza ghasia wakipuliza gesi ya moto kudhibiti fujo nje ya Uwanja wa Maracana
Fred akifunga
Fred alifunga dakika ya pili tu bao la kwanza
Mwanzo mzuri: Fred akishangilia na Neymar