// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); BILIONEA BAKHRESA APIGA HATUA KUBWA, ANUNUA TIMU YA LIGI KUU ZANZIBAR, SASA NI AZAM NCHI NZIMA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE BILIONEA BAKHRESA APIGA HATUA KUBWA, ANUNUA TIMU YA LIGI KUU ZANZIBAR, SASA NI AZAM NCHI NZIMA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Thursday, July 04, 2013

    BILIONEA BAKHRESA APIGA HATUA KUBWA, ANUNUA TIMU YA LIGI KUU ZANZIBAR, SASA NI AZAM NCHI NZIMA

    Chukua Tano; Bilionea Alhaj Said Salim Awadh Bakhresa, baada ya Azam FC sasa aja na timu ya pili Ligi Kuu Zanzibar
    Na Salum Vuai, Zanzibar, IMEWEKWA JULAI 4, 2013, SAA 3:37 ASUBUHI 
    SIKU chache baada ya Shirika la Bandari Zanzibar kujivua jukumu la kuiendesha timu yake ya soka Bandari SC, uongozi wa timu hiyo umeamua kuiuza nafasi yake kwa makampuni ya S.S. Bakhresa yanayomiliki klabu ya Azam FC ya Dar es Salaam.
    Uamuzi wa kuuza daraja hilo la ligi kuu kwa matajiri hao wa ngano, ‘ice cream’ na boti za Azam Marine, umefikiwa katika mkutano wa wanachama na uongozi wa timu na shirika, uliofanyika Julai 1, mwaka huu.
    BIN ZUBEIRY imefanikiwa kuitia mikononi nakala ya barua iliyoandikwa na Katibu wa Bandari SC kwenda Chama cha Soka Zanzibar (ZFA), ya Julai 1, 2013, yenye namba ya kumbukumbu ZPC/BSC/VOL1/40/2013, kuelezea uamuzi wake huo.
    Imeelezwa kuwa, mkutano huo ulishirikisha viongozi wa shirika, timu na wanachama, ambao jumla yao walikuwa 71, na baadae kutia saini muafaka wa kupiga bei daraja lao kwenye ligi kuu ya Zanzibar.
    Aidha, orodha yenye majina ya wanachama hao, imeambatanishwa na barua hiyo kwenda ZFA Taifa.
    Baada ya kupata taarifa hiyo, BIN ZUBEIRY iliwasiliana na Katibu Mkuu wa Azam FC, Nassor Idrissa Mohammed ‘Father’, ambaye alikiri kuwa uongozi wa timu yake umeshakaa mezani na wenzao wa Bandari, na tayari wamekubaliana kwa mauziano hayo.
    Hata hivyo, alisema kwa sasa wamewapa kazi wanasheria wao, kuangalia sheria na kanuni za ZFA zinaelekeza nini kabla kumalizana na Bandari.
    “Kimsingi tumeshakubaliana na wenzetu wa Bandari na wameafiki kutuuzia nafasi yao kwenye ligi kuu ya Zanzibar. Unaweza kuandika hivyo, yaliyobaki ni mambo ya kisheria zaidi ambayo ninaamini yatatengemaa karibuni”, alifafanua Mohammed ‘Father’.
    Kuhusu tetesi kwamba awali walitaka kununua daraja la klabu ya Malindi iliyoteremka daraja kutoka ligi kuu hadi la kwanza taifa, Idrissa alisema hawana mpango huo kwani lengo lao ni kucheza ligi kuu moja kwa moja.
    Naye Katibu wa Bandari SC Makame Silima Makame, akizungumza hatima ya wachezaji wa kikosi cha timu yake baada ya kuuza daraja lao, alisema wanakusudia kununua nafasi katika ligi ya daraja la pili msimu ujao, ili waendelee kuwemo kwenye soka.
    Hata hivyo, alisema hatua hiyo itafanyika baada ya kumaliza mchakat wa kuuza daraja lao kwa Azam FC.
    Taarifa ambazo BIN ZUBEIRY imezipata, zimesema kuwa, huenda Azam haitahitaji hata mchezaji mmoja wa Bandari, lakini Katibu Mkuu wa ZFA Kassim Haji Salum alisema hilo litafafanuliwa zaidi katika kanuni za chama hicho, zinazoendelea kufanyiwa marekebisho.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: BILIONEA BAKHRESA APIGA HATUA KUBWA, ANUNUA TIMU YA LIGI KUU ZANZIBAR, SASA NI AZAM NCHI NZIMA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top