// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); AZAM WAIPA SIMBA SC MILIONI 331 JIONI HII DAR ES SALAAM, RAGE APAGAWA KWA FURAHA NA KUSEMA YOTE - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE AZAM WAIPA SIMBA SC MILIONI 331 JIONI HII DAR ES SALAAM, RAGE APAGAWA KWA FURAHA NA KUSEMA YOTE - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
    Thursday, July 18, 2013

    AZAM WAIPA SIMBA SC MILIONI 331 JIONI HII DAR ES SALAAM, RAGE APAGAWA KWA FURAHA NA KUSEMA YOTE

    Na Mahmoud Zubeiry, IMEWEKWA JULAI 18, 2013 SAA 3:19 USIKU 
    KAMPUNI ya mpya ya Habari nchini, Azam Media Group, leo imeingia Mkataba wa miaka mitatu wenye thamani ya Sh. Milioni 331 na klabu ya Simba ya Dar es Salaam kwa ajili ya kurusha kipindi maalum cha klabu hiyo, kitakachojulikana kama Simba TV kupitia kituo kipya cha Televisheni, Azam TV.
    Mwenyekiti wa Simba SC, Alhaj Ismail Aden Rage, kwa pamoja na Katibu, Evodius Mtawala na Mjumbe wa Baraza la Wadhamini, Hamisi Kilomoni waliiwakilisha klabu hiyo katika utiaji saini wa Mkataba huo mnono kwenye ukumbi wa Kibo, jengo la PSPF, Dar es Salaam.
    Utajiri huu; Mwenyekiti wa Simba, Alhaj Ismail Aden Rage (kushoto) akipeana mikono na Mkueugenzi wa Azam Media, Abubakar Bakhresa kulia baada ya kuingia Mkataba huo. Katikati ni Mwanasheria wa Azam Media, Shani Chrstoms.

    Upande wa Azam uliwakilishwa na Mkurugenzi Mkuu, Abubakar Bakhresa, Meneja Mkuu, Said Mohamed na Mwanasheria, Shani Christoms ambao waliikabidhi Simba SC hundi za fedha hizo kwenye hafla hiyo.
    Meneja wa Azam Media, Mzee Said alisema kwamba Mkataba huo ni mwanzo tu, lakini kampuni hiyo imejipanga kusaidia zaidi soka ya Tanzania kwa kuingia mikataba mingi yenye manufaa kwa mchezo huo nchini.
    Mkataba mnono wallahi; Rage akiusoma Mkataba huku akifurahi pembeni ya Abubakar Bakhresa

    Mzee Said alisema Azam Media inaleta mapinduzi na ukombozi katika medani ya michezo Tanzania na kwamba Watanzania wakae tayari kushuhudia mambo makubwa muda si mrefu kupitia Azam TV.
    Wanamwaga wino;Shani kulia akiwashuhudia Rage na Mzee Kilomoni wakisani Mkataba
    Inakuja hivi karibuni; Bango la Azam TV lenye ujumbe inakuja hivi karibuni 
    Alhaj Rage, pamoja na kuwashukuru Azam Media kwa Mkataba huo mnono, alisema klabu inategemea kujikomboa zaidi kiuchumi kutokana na mikataba ya udhamini kama hiyo na muda si mrefu wataingia mikataba mingine itakayokuza zaidi pato la klabu.
    Hundi za Milioni 331; Kutoka kulia Abubakar Bakhresa, Mzee Said Mohamed, Shani na Rage akiwa ameshika hundi zake

    “Nimesikia pia mnataka kununua haki za Televisheni za Ligi Kuu ya Tanzania Bara, mimi nasema karibuni na katika hilo, natoa angalizo, mkinunua haki za TV za Ligi Kuu, naomba mtoe fungu sawa kwa kila klabu, hakuna kubagua eti huyu apate kidogo, yule apate zaidi, hapana,”.
    Mbele ya bango; Kutoka kulia Abubakar, Mzee Said, Shani, Rage, Mzee Kilomoni na Mtawala
    Fedha hizi tunasajili mshambuliaji mwingine; Rage akiteta na Katibu wake, Mtawala mbele ya Mzee Kilomoni
    Tunaleta mapinduzi na ukombozi katika soka ya Tanzania; Mzee Said akizungumza pembeni ya Abubakar Bakhresa

    “Lazima mpira wa miguu katika nchi hii maendeleo yafike kila sehemu na tuondoe ubinafsi wa kujifikiria eti sisi Simba ndiyo tupate zaidi, hapana. Hiyo si haki, lazima na zile klabu ndogo pia nazo zinufaike sawa na sisi kwa kuwa tunacheza ligi moja,”alisema Rage ambaye pia ni Mbunge wa Tabora Mjini (CCM).
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: AZAM WAIPA SIMBA SC MILIONI 331 JIONI HII DAR ES SALAAM, RAGE APAGAWA KWA FURAHA NA KUSEMA YOTE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry