IMEWEKWA JULAI 19, 2013 SAA 2:34 USIKU
KLABU ya Arsenal sasa imehamishia ndoana zake kwa kiungo wa Chelsea, Juan Mata majira haya ya joto.
Mustakabali wa Mspanyola huyo Stamford Bridge umekuwa haueleweki tangu kurejea kwa Jose Mourinho.
Na BIN ZUBEIRY inafahamu The Gunners imefufua mpango wa kumsajili mchezaji huyo wa zamani wa Valencia.
Mtu anayetakiwa: Juan Mata anatakiwa na Arsenal
Kocha Arsene Wenger alikaribia kumsajili Mata mwaka 2011, lakini Chelsea wakaipiga bao The Gunners kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25.
Mata amekuwa mmoja wa wachezaji bora Ligi Kuu, akiiwezesha Chelsea kutwaa Ligi ya Mabingwa Ulaya, Europa League na Kombe la FA tangu atue Darajani.
Chelsea imesema mchezaji huyo hauzwi majira haya ya joto, lakini Arsenal itaendelea kufuatilia kwa makini juu ya mustakabali wa mchezaji huyo.
Mata akicheza na maji wakati wa mapumziko Ibiza
Taarifa zilizopatikana mapema wiki hii zilisema kwamba Mata au David Luiz mmoja wao atatumiwa kufanikisha usajili wa mshambuliaji wa Manchester United, Wayne Rooney kutua Chelsea.
Lakini Mourinho alipuuzia taarifa hizo, akisema hakuna nafasi au hata mchezaji wa kuuzwa majira haya ya joto.
Mustakabali wa Mata umekuwa haueleweki tangu Jose Mourinho arejee Chelsea
Nyota wa mavitu: Mata alichaguliwa Mchezaji Bora wa Mwaka wa Chelsea kwa msimu wa pili mfululizo
Mata amefunga mabao 11 Ligi Kuu msimu uliopita na kutoa pasi 13 za mabao, iliyomfanya awe Mchezaji Bora wa Mwaka wa klabu kwa mara ya pili mfululizo.
Arsenal pia inawataka washambuliaji wa Liverpool, Luis Suarez, wa Manchester United, Wayne Rooney na wa Real Madrid, Gonzalo Higuain majira haya joto.