IMEWEKWA JUNI 22, 2013 SAA 3:30 USIKU
WANASHERIA Lionel Messi wamesema madai ya ukweipaji kodi ni uzushi, lakini watafanya chochote kuyamaliza kama itakavyohitajiwa.
Mwanasheria, Juarez Veciana amesema katika taarifa yake kwamba mashitaka ya mshambuliaji huyo wa Barcelona dhidi ya serikali ya Hispania hayana ukweli.
Messi na baba yake, Jorge wametakiwa kufika mahakamani katika mji wa Gava, karibu na Barcelona Septemba 17 kujibu mashitaka ya ukwepaji kodi Pauni Milioni 3.4 kati ya mwaka 2007 na 2009.
Malalamiko: Messi, akifanya manunuzi katika duka la Dolce na Gabbana Jijini Milan, atalipa faini ya Pauni Milioni 3.4
Kesi: Nyota wa Barcelona anakabiliwa na kesi ya kukopa kodi
"Tunakubali kwamba mteja wetu atalipa kiasi anachodaiwa,"alisema mwanasheria wa Messi. "Lakini tunaamini mteja wetu amekwishalipa kiasi kinachodaiwa.'
Mwendesha mashitaka wa amedai Messi na baba yake, walizitumia kampuni za Belize na Uruguay kukwepa malipo ya kodi za mapato kutokana na haki ya picha.
Malalamiko hayo yanawafanya wadhamini wa Messi kuchunguzwa. Inawahusisha Barcelona, Adidas, Danone, Konami, Procter & Gamble, Pepsi-Cola na Telefonica, na wengineo.
Wakikutwa na hatia, Messi na baba yake watalipishwa faini ya asilimia 150 ya mapato ambayo hawakulipia kodi na kutupwa jela kati ya miaka miwili na sita.