IMEWEKWA JUNI 21, 2013 SAA 7:00 USIKU
MSHAMBULIAJI Fernando Torres amefunga mabao manne pamoja na kukosa penalti wakati Hispania ikiifumua 10-0 Tahiti katika mchezo wa Kundi B Kombe la Mabara.
Alifunga mabao hayo katika dakika za tano, 33, 57 na 78 wakati David Villa alipiga Hat-trick katika dakika za 39,49 na 64, David Silva akafunga mawili dakika za 31 na 89 na Juan Mata pia akafunga dakika ya 66 kuiwezesha Hispania kupaa kileleni mwa Kundi B mbele ya Nigeria, ambao muda huu wanamenyana na Uruguay.
Kikosi cha Hispania kilikuwa: Reina, Albiol, Azpilicueta, Ramos/Navas dk46, Monreal, Martinez, Cazorla/Iniesta dk76, Silva, Villa, Torres na Mata/Fabregas dk69.
Tahiti: Roche, Ludivion, Vallar, Lemaire/Vero dk73, Aitamai, J Tehau, A Tehau/T Tehau dk53, Vahirua, Caroine, Bourebare/L Tehau dk69 na Chong Hue.
Tunapaa: Fernando Torres alikuwa moto usiku huu
Nami pia: Mshambuliaji wa Barcelona, David Villa alifunga pia
Torres akifunga
KUNDI B KOMBE LA MABARA
Timu | Mechi | Kushinda | Sare | Kufungwa | Mabao ya kufunga | Mabao ya kufungwa | Pointi |
---|---|---|---|---|---|---|---|
Spain | 2 | 2 | 0 | 0 | 12 | 1 | 6 |
Nigeria | 1 | 1 | 0 | 0 | 6 | 1 | 3 |
Uruguay | 1 | 0 | 0 | 1 | 1 | 2 | 0 |
Tahiti | 2 | 0 | 0 | 2 | 1 | 16 | 0 |