IMEWEKWA JUNI 26, 2013 SAA 4:10 USIKU
MRENO Cristiano Ronaldo anaweza kurejea Manchester United baada ya kugundulika atakuwa na mkutano na viongozi wa klabu hiyo ya Old Trafford ndani ya siku tatu zijazo.
Nyota huyo wa Real Madrid amekuwa akihusishwa na kurejea England baada ya kupitia msimu wa bila furaha Bernabeu, lakini ilitarajiwa kuwasili kwa kocha mpya, Carlo Ancelotti kungemfanya abaki Hispania.
Na gazeti la Hispania, El Pais limeripoti kwamba nahodha huyo wa Ureno atakutana na viongozi wa United, kabla hajaenda kuanza maandalizi ya msimu mpya Madrid.
Sakata la kuhama: Ikiwa United itafanikiwa kumnasa Ronaldo, utakuwa usajili babu kubwa zaidi majira haya ya joto
JINSI ALIVYOKUWA MTAMBO WA MABAO
Manchester United
LIGI: Mechi 196, mabao 84
KOMBE: Mechi 38, mabao 17
ULAYA: Mechi 55, mabao 16
JUMLA: Mechi 189, mabao 117
Real Madrid
LIGI: Mechi 135, mabao 146
KOMBE: Mechi 20, mabao 17
ULAYA: Mechi 40, mabao 35
JUMLA: Mechi 195, mabao 198
Kwa kuwa FIFA inazuia klabu kufanya mazungumzo na wachezaji walio ndani ya Mikataba na klabu zao, pande zote zimejipanga kukana kufanya mazungumzo, ambayo itamsaidia sana kocha mpya, David Moyes kuelekea msimu ujao.
Lakini Ancelotti amesema wakati akitambulishwa kuwa kocha mpya wa Madrid leo kwamba: "Cristiano ni mchezaji mkubwa na ninajivunia kufanya naye kazi.
"Nimewakochi Zidane, Ronaldo na Ronaldinho, na ninajivunia kumuongeza na yeye.'
Alipoulizwa kuhusu Radamel Falcao, mchezaji aliyekuwa anawaniwa na Madrid ambaye amesaini Monaco, Ancelotti alisema: "Ni mchezaji mzuri, lakini kuna Ronaldo, Higuain na Benzema,"alisema.