IMEWEKWA JUNI 2, 2013 SAA 12:10 JIONI
KOCHA Manuel Pellegrini amesema ataanza mpango wa kuhamia Manchester City Jumatatu.
Mwalimu huyo mwenye umri wa miaka 59 raia wa Chile aliwaaga Malaga kwa kipigo cha 4-1 kutoka kwa Barcelona katika mchezo wa mwisho wa Primera Division jana.
Pellegrini alisema baada ya kipigo hicho: "Tutaona kuanzia Jumatatu mustakabali wangu unapoelekea. Wakati makubaliano yatakapofikiwa, tutasema kitu fulani kufafanua,"alisema.
Manuel Pellegrini alikiona cha moto kwa Barcelona katika mchezo wake wa mwisho Malaga