IMEWEKWA JUNI 30, 2013 SAA 4:00 USIKU
KOCHA mpya wa Manchester City, Manuel Pellegrini amewasili England tayari kurithi rasmi mikoba ya Roberto Mancini Uwanja wa Etihad.
Raia huyo wa Chile alitumia muda fulani kushangaa shangaa maeneo ya Jiji la Manchester na kuchukua suti iliyo sawa yake katika duka la Hugo Boss kabla ya kutambulishwa na kukabidhiwa jezi ya bluu.
Alikuwa na wasaidizi wake akiwemo Ruben Cousillas na kocha wa ufiti, Jose Cabello.
Ametua England: Manuel Pellegrini akionyesha jezi ya Manchester City kwa mara ya kwanza
Pellegrini akiwasili Uwanja wa Ndege wa Manchester na wasaidizi wake
Akiita teksi: Pellegrini katika jiji la Manchester akizungumza kiingereza kizuri
Mwalimu huyo mwenye umri wa miaka 59, amejiunga na timu hiyo kutoka Malaga, na anatakiwa haraka kuhakikisha timu inafanya vizuri ili kuwafurahisha mashabiki na watu wa klabu hiyo.
Mpinzani wake mpya Manchester, David Moyes, anaanza kazi kesho United na Pellegrini atatazamiwa kumpiga bao kuanzia katika usajili.
City tayari imepigwa bao na Real Madrid katika saini ya kijana wa zamani wa Pellegrini, Isco, ambaye aling'ara katika Kombe la Euro kwa vijana chini ya umri wa miaka 21 nchini Israel akiwa na Hispania iliyotwaa ubingwa.
Salamu ya kwanza: Pellegrini alikutana na msafara kutoka Manchester City katika saa zake za mwanzoni asubuhi
Suti yako! akiangalia suti