IMEWEKWA JUNI 21, 2013 SAA 12:00 ASUBUHI
MSHAMBULIAJI Diego Forlan usiku wa kuamkia leo amesherehekea mechi yake ya 100 Uruguay kwa kufunga bao la ushindi timu yake ikishinda 2-1 dhidi ya Nigeria kwenye Kombe la Mabara mjini Salvador.
Forlan alifunga mwanzoni mwa kipindi cha pili baada ya John Obi Mikel kuisawazishia Nigeria dakika ya 37 kufuatia Uruguay kufunga bao la kuongoza dakika ya 19 kupitia kwa Diego Lugano.
Forlan akishangilia na mwenzake
Diego Lugano akipongezwa na wenzake
Matokeo hayo yanafanya timu mbili katika Kundi hilo, B zilingane kwa pointi, tatu kila moja baada ya kucheza mechi mbili, lakini ikiwa imebakiza mechi na Tahiti, Uruguay iko katika nafasi kubwa ya kusonga mbele pamoja na Hispania, yenye pointi sita na itacheza na Nigeria katika mechi ya mwisho ya kundi hilo.
KUNDI B KOMBE LA MABARA
Timu | Mechi | Kushinda | Sare | Kufungwa | Mabao ya Kufungwa | Mabao ya kufungwa | Pointi |
---|---|---|---|---|---|---|---|
Hispania | 2 | 2 | 0 | 0 | 12 | 1 | 6 |
Nigeria | 2 | 1 | 0 | 1 | 7 | 3 | 3 |
Uruguay | 2 | 1 | 0 | 1 | 3 | 3 | 3 |
Tahiti | 2 | 0 | 0 | 2 | 1 | 16 | 0 |
John Obi Mikel (kulia) akishangilia baada ya kufunga
Martin Caceres wa Uruguay akimdhibiti Ahmed Musa