IMEWEKWA JUNI 18, 2013 SAA 6:20 USIKU
TIMU ya taifa ya Nigeria imeifumua kwa mabao 6-1 Tahiti katika Kombe la Mabara usiku huu.
Jonathan Tehau aliifungia Tahiti, lakini Nnamdi Oduamadi akaifungia Super Eagles mabao matatu peke yake.
Mabingwa wa Oceania, Tahiti, wakiwa na mchezaji mmoja tu wa kulipwa kikosini, walikuwa wana mwanzo mgumu katika mchezo huo wa Kundi B wakati mpira ulipomgonga refa na kumkuta mchezaji wa Nigeria, Uwa Echiejile ambaye alifunga kwa shuti la kubabatiza dakika ya tano.
Nigeria ikapata bao la pili lililofungwa na Oduamadi dakika tano baadaye.
Tahiti iliwanua vitini mashabiki wake wakati Tehau alipofunga bao dakika ya 54.
Lakini Nigeria iliendelea kung'ara wakati Tehau alipojifunga kabla ya Oduamadi kukamilisha Hat-trick yake na Echiejile akafunga bao lake la pili kwenye mchezo huo.
Kikosi cha Nigeria kilikuwa: Enyeama, Ambrose, Omeruo, Oboabona, Echiejile, Ogude, Mikel, Mba, Oduamadi, Ujah na Musa.
Tahiti: Samin, A Tehau, Vahirua, Ludivion, Caroine, Bourebare, Vallar, Chong Hue, Aitamai, J Tehau na Simon.
Nnamdi Oduamadi (kulia) akishangilia baada ya kufunga dhidi ya Tahiti
Nnamdi Oduamadi wa Nigeria akifunga
Jonathan Tehau akiifungia Tahiti
Jonathan Tehau akifunga
Anashangilia
Tehau
Oduamadi akifunga bao la tano
Saluti: Wachezaji wa Tahiti