// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); NEYMAR: HATUIHOFII HISPANIA, INGAWA KWELI INAPEWA NAFASI YA KUTWAA KOMBE KESHO - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE NEYMAR: HATUIHOFII HISPANIA, INGAWA KWELI INAPEWA NAFASI YA KUTWAA KOMBE KESHO - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Saturday, June 29, 2013

    NEYMAR: HATUIHOFII HISPANIA, INGAWA KWELI INAPEWA NAFASI YA KUTWAA KOMBE KESHO

    IMEWEKWA JUNI 29, 2013, SAA 3:17 USIKU
    NYOTA wa Brazil, Neymar anaamini Hispania inapewa nafasi kubwa ya kutwaa Kombe la Mabara katika Fainali itakayopigwa kesho, lakini amesema timu yake haiwahofii mabingwa hao wa Ulaya na Dunia.
    Hispania inaingia kwenye fainali hiyo kesho, ikitazamiwa kushinda taji hilo kwa mara ya kwanza na kuendeleza mafanikio yao ya miaka ya karibuni katika soka, wakitwaa mfululizo mataji ya Euro na Kombe la Dunia.
    Mafanikio hayo yameifanya La Roja ishike nafasi ya kwanza katika viwango vya soka duniani na licha ya kwamba Brazil inapewa nafasi kutokana na kucheza nyumbani, Neymar amesema kikosi cha Vicente Del Bosque ni tishio.
    Neymar
    Mazoezi yanajenga usahihi: Neymar (katikati), ambaye hivi karibuni amesaini Barcelona, akiwa na mpira mguuni mwake

    Pamoja na hayo, mshambuliaji huyo ambaye atacheza Ligi Kuu ya Hispania msimu ujao baada ya kujiunga na Barcelona mapema majira haya ya joto, pia ana matumaini na timu yake inaweza kuweka rekodi ya kutwaa kwa mara ya tatu mfululizo Kombe la Mabara na mara ya nne kwa ujumla.
    "Wao (Hispania) ni timu nzuri duniani na wanapewa na nafasi,"alisema mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21.
    "Lazima tucheze soka bila woga. Tunacheza na timu bora duniani kwa sasa, lakini pia tuna wachezaji wazuri katika timu ya taifa ya Brazil,".
    Jo and Scolari
    Maelekezo: Kocha wa Brazil, Luiz Felipe Scolari (kulia) akizungumza na mshambuliaji wa zamani wa Everton na Man City, Jo

    Kocha wa Brazil, Luiz Felipe Scolari amesema kikosi chake kina uwezo wa kuibwaga Hispania.
    "Tunacheza na Hispania tukiheshimu ubora wao, lakini pia kujaribu kuonyesha uwezo wetu na vipaji,"alisema.
    "Tumefika Fainali na tuna ubora wa kutosha kuwabwaga,".
    Nchi hizo mbili zinakutana kwa mara ya kwanza tangu zitoke 0-0 katika mchezo wa kirafiki mjini Vigo mwaka 1999. Mara ya mwisho, Hispania ilipokutana na Brazil Uwanja wa Maracana walifungwa mabao 6-1 - mwaka 1950.
    Brazil squad
    Samba: (kutoka kushoto) Marcelo, Oscar, Fred, Neymar, David Luiz na Hulk katika mazoezi ya Brazil mjini Rio

    Timu zote zimeonyesha ni timu mwaka huu katika Kombe la Mabara, Brazil ikishinda mechi zake zote nne hadi sasa, wakati Hispania walishinda mechi zao zote tatu za kundi lao, kabla ya kuing'oa kwa matuta Italia kwenye Nusu Fainali kali katikati ya wiki.
    Andres Iniesta
    Andres Iniesta ataiongoza Hispania kesho
    Marcelo and Neymar
    Wamemaliza siku yao: Nyota wa Real Madrid, Marcelo (kulia) akiburuza kipozeo baada ya mazoezi huku Neymar akimuangalia
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: NEYMAR: HATUIHOFII HISPANIA, INGAWA KWELI INAPEWA NAFASI YA KUTWAA KOMBE KESHO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top