IMEWEKWA JUNI 23, 2013 SAA 9:30 USIKU
MABAO ya Dante dakika ya 45, Neymar 55 na mawili ya Fred dakika za 66 na 88 yameipa Brazil ushindi waliostahili wa 4-2 dhidi a Italia usiku huu na kufuzu Nusu Fainali ya Kombe la Mabara ikishinda mechi zote katika Kundi A.
Italia ilipata mabao yake kupitia kwa Giaccherini dakika ya 51 na Chiellini dakika ya 71.
Kikosi cha Brazil kilikuwa; Julio Cesar, Dani Alves, Thiago Silva, Luiz/Dante dk33, Marcelo, Gustavo, Hernanes, Hulk/Fernando dk76, Oscar, Neymar/Bernard dk68 na Fred.
Italia: Buffon, Abate/Maggio dk30, Bonucci, De Sciglio, Chiellini, Candreva, Aquilani, Marchisio, Montolivo/Giaccherini dk26, Diamanti/El Shaarawy dk71 na Balotelli.
Na tena: Neymar ameifungia tena Brazil katika ushindi wa 4-2 dhidi ya Italia
Neymar akifunga
Emanuele Giaccherini akimtungua Julio Cesar baada ya kupokea pasi ya Mario Balotelli
MSIMAMO KUNDI A KOMBE LA MABARA
Timu | Mechi | Kushinda | Sare | Kufungwa | Mabao ya kufunga | Mabao ya kufungwa | Pointi |
Brazil | 3 | 3 | 0 | 0 | 9 | 2 | 9 |
Italy | 3 | 2 | 0 | 1 | 8 | 8 | 6 |
Mexico | 3 | 1 | 0 | 2 | 3 | 5 | 3 |
Japan | 3 | 0 | 0 | 3 | 4 | 9 | 0 |
Katika mchezo mwingine wa kundi hilo, Javier Hernandez alifunga mabao mawli na kukosa penalti Mexico ikiifunga Japan 2-1 na kumaliza katika nafasi ya tatu kwenye Kundi A.
Bao la Japan lilifungwa na Shinji Okazaki na sasa Brazil inaungana na Italia kusonga Nusu Fainali.
Nyota: Javier Hernandez amefunga mawili dhidi ya Japan