IMEWEKWA JUNI 2, 2013 SAA 12: 50 ASUBUHI
KOCHA Jose Mourinho jana aliwaaga mashabiki wa Real Madrid katika mchezo wa mwisho wa La Liga alipokea kelele za kushangiliwa na kuzomewa wakati timu yake ikiifunga Osasuna 4-2 Uwanja wa Bernabeu.
Lakini kulitokea sintofahamu kuhusu mustakabali wa mchezaji anayewaniwa na Manchester United na Chelsea, Cristiano Ronaldo, ambaye aliikosa mechi hiyo kutokana na kuwa majeruhi.
Kocha huyo Mreno alitoa taarifa fupi ya kuaga katika tovuti ya Madrid saa chache kabla ya mechi na Osasuna.
Baada ya mechi, Mourinho, ambaye anatarajiwa kukamilisha uhamisho wake wa kurejea Chelsea msimu ujao, aliwapungia mono mashabiki kuwaaga kabla ya kuondoka uwanjani.
Mourinho akiwa amezungukwa na wapiga picha jana Bernabeu
Kushangiliwa na kuzomewa: Mourinho alipigiwa kelele za kushangiliwa na kuzomewa pia jana
"Nawatakia furaha mashabiki wote Real Madrid siku zijazo," alisema Mourinho. "Nataka kuwashukuru mashabiki wengi kwa sapoti yao, na ninaheshimu wengine walionibeza. Narudia, furaha kwa wote, na juu ya hayo, afya njema. Hala (mbele) Madrid!"
Heshima: Mashabiki wa Real Madrid wakipeperusha bendera ya Mourinho katika mechi hiyo
Mashabiki wa Real wakiwa wamebeba ujumbe wa 'Tunakushuuru' kumuaga Kocha huyo Mreno
Mourinho akipunga mkono kuaga Madrid
Mourinho, ambaye katika maisha yake ya ukocha anajivunia kutwaa mataji mawili ya Ligi ya Mabingwa na ubingwa wa Ligi za Ureno, England, Italia na Hispania Spain anatarajiwa kurejea Chelsea msimu ujao.
Baada ya kushinda Kombe la Mfalme katika msimu wake wa kwanza na Ligi Kuu ya Hispania katika msimu wa pili, Mourinho na klabu zilikubaliana kuachana baada ya msimu huu wa tatu.
Mourinho amekuwa akishambuliwa mno kwa kumuweka benchi Nahodha na kipa Iker Casillas msimu huu na akionekana kuwapendelea baadhi ya wachezaji kama Pepe.
Cristiano Ronaldo hakucheza jana sababu ya majeruhi
Ronaldo akiwapungia mkono mashabiki Bernabeu
Gonzalo Higuain aliifungia bao la kwanza Real Madrid jana
Michael Essien, aliyefanya kazi na Mourinho Chelsea, aliifungia bao la pili Madrid kabla ya kupumzishwa
Wachezaji wengine wa Madrid wamemtakia kila la heri Mourinho.
Katika mchezo wa jana, Gonzalo Higuain aliifungia Madrid bao la kuongoza dakika ya 35, kabla ya Michael Essien kufunga la pili dakika nne baadaye.
Osasuna ilisawazisha kupitia kwa Roberto Torres na Alvaro Cejudo.
Karim Benzema akaisawazishia Real zikiwa zimesalia dakika 20 kabla ya bao la dakika za lala salama la Jose Callejon kuihakikishia ushindi Real katika mchezo huo wa mwisho wa La Liga na uliohitimisha miaka mitatu ya Mourinho Bernabeu.