IMEWEKWA JUNI 27, 2013 SAA 9:53 ALASIRI
BAADA ya kumnasa Carlos Tevez kutoka Manchester hadi Turin, Juventus sasa inataka kubeba nyota mwingine wa City, beki Aleksandar Kolarov naye ahamie Italia.
BIN ZUBEIRY kutoka Sportsmail iliandika mapema mwezi huu kwamba Kibibi Kizee hicho kimefufua mpango wake wa kumsajili beki huyo wa kimataifa wa Serbia na sasa The Sun linaripoti kwamba, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 yupo njiani kwenda klabu hiyo.
Uhamisho huo utamfanya aungane mshambuliaji Muargentina, Tevez, ambaye alishikishwa jezi ya Juve jana baada ya kukubali uhamisho wa Pauni Milioni 10 kutua kwa mabingwa wa Serie A, ingawa atalazimika kutumikia adhabu ya kufanya kazi za kijamii England kwa saa 250.
Amezungumza na Juve: Kolarov anaweza kuungana na Tevez (chini, kulia) Italia
Kolarov alisajiliwa kutoka Lazio kwa ada ya uhamisho ya Pauni Milioni 16 miaka mitatu iliyopita, na City inaweza kuwa tayari kumruhusu kurejea Italia kwa hasara ya Pauni Milioni 7, kutokana na Gael Clichy kufanikiwa kuwa chaguo la kwanza katika beki ya kushoto ya klabu hiyo.
"Nipo kwenye mawasiliano na Antonio Conte wa Juventus, hivyo tutaona kitakachotokea," Kolarov aliliambia The Sun.
"Nataka uhakika wa kucheza,".
Kibibi Kizee kipya: Tevez akipeperusha jezi yake mpya ya Juve kwa mashabiki mjini Turin jana