IMEWEKWA JUNI 28, 2013 SAA 8:39 MCHANA
KLABU ya Barcelona imekubali kusaini Mkataba mpya na Rafael 'Rafinha' Alcantara ili kuendelea kuishi na mdogo huyo wa Thiago hadi mwaka mwaka 2016.
Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 20, sasa anaweza kutumika kama ushawishi kwa kaka yake, Thiago na klabu hiyo Katalunya ili asikubali kuhamia Manchester United anakotakiwa abaki.
Awali, Rafinha alihusishwa na kuhamia Ligi Kuu England ambako kaka yake, Thiago pia yuko njiani kuhamia.
Mkataba mpya: Rafinha Alcantara amesaini Mkataba wa kuendeela kukipiga Barcelona
Pigo: Habari hizi zinaweza kuwa pigo kwa Manchester United ambayo ilitarajia Rafinha kuhamia England angesaidia wao kumpata kaka yake, Thiago
Lakini klabu hiyo ya Catalan inatarajiwa kuwa na mazungumzo na kiungo huyo anayetaka kuondoka, ambaye amekubali mshahara wa Pauni Milioni 5.5 kwa mwaka kutoka United baada ya kushindwa kupata uhakika wa namba katika kikosi cha kwanza msimu uliopita.
Mkataba wake unasema anatakiwa acheze kwa asilimia 60 kikosi cha kwanza, kitu ambacho hakikufikiwa.
Barcelona inataka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 abaki na imemuhakikishia atakuwa kiongozi wa timu baada ya Xavi na Iniesta kueonekana wanalekea 'uzeeni'.
Rafinha, ambaye ameamua kufuata uraia wa baba yake, Mazinho Brazil, badala ya Hispania kwa mama, alitwaa Kombe la Dunia na Brazil na ameichezea mechi 36 Barcelona B msimu uliopita, akifunga mabao 10 kikosi hicho cha wachezaji wa akiba kikishika nafasi ya nane Ligi ya Segunda.
Kubadili uraia: Rafinha amebadili uraia kutoka Hispania hadi Brazil