// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); ITV WAPIGA BAO TUZO ZA KILI, KUONYESHA MZIGO 'LIVE BILA CHENGA' - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE ITV WAPIGA BAO TUZO ZA KILI, KUONYESHA MZIGO 'LIVE BILA CHENGA' - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Sunday, June 02, 2013

    ITV WAPIGA BAO TUZO ZA KILI, KUONYESHA MZIGO 'LIVE BILA CHENGA'

    Kavishe akizungumza mchana wa leo Roots
    Na Princess Asia, IMEWEKWA JUNI 2, 2013 SAA 6:30 MCHANA
    TELEVISHENI kongwe nchini inayonasa bila mawimbi, ITV imepewa tenda ya kuonyesha moja kwa moja onyesho la tuzo za muziki Tanzania, Kili Music Award litakalofanyika Juni 8,  mwaka huu kwenye ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam.
    Akizungumza na Waandishi wa Habari leo mchana katika ukumbi wa Roots, Masaki, Dar es Salaam, Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, George Kavishe amesema kwamba sababu za kuichagua ITV ni kuamini wanaweza kufanya kazi hiyo kwa ufanisi.
    Kavishe katika jukwaa la KTMA

    Pamoja na kurushwa live kupitia ITV, Kavishe amesema kwamba onyesho hilo litaonyeshwa live katika sehemu tatu tofauti nchini, ambazo wameziteua.
    Alizitaja sehemu hizo kuwa ni Mwanza eneo la Mabatini, Temeke Uwanja wa Taifa na Kilimanjaro CCM Mkoa.
    Kavishe alisema zoezi la kupigia kura wasanii kuelekea tuzo hizo zinazokwenda na kaulimbiu ya Kikwetukwetu mwaka huu lilifungwa Mei 31, mwaka huu. 
    Kuhusu burudani katika usiku huo, Kavishe alisema kwamba wasanii wa sasa wataimba nyimbo za wasanii wa zamani na wasanii wa zamani wataimba nyimbo za wasanii wa sasa.
    “Kutakuwa na kitu tofauti sana upande wa burudani, ambacho kitapendeza na kuvutia sana, kwa ujumla maandalizi yako vizuri na tunatarajia mambo mazuri siku hiyo,”alisema Kavishe.     
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: ITV WAPIGA BAO TUZO ZA KILI, KUONYESHA MZIGO 'LIVE BILA CHENGA' Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top